Msimu huu kumeanza na moto!

Muktasari:
MZUNGUKO wa kwanza Ligi Kuu Bara umekamilika na kushuhudia rekodi mbalimbali zilizokwekwa tofauti na msimu uliopita miongoni mwa rekodi hizo msimu uliopita mzunguko wa kwanza ulikamilika kwa kushuhudia kufungwa mabao kumi wakati msimu huu mabao 20. Katika mzunguko wa kwanza msimu huu zilipatikana penalti nne - mbili kati ya hizo zilifungwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama dhidi ya Geita; mshambuliaji wa Coastal Union, Moubarack Hamza dhidi ya KMC.

Penalti mbili zilikoswa na straika wa Yanga, Fiston Mayele dhidi ya Polisi Tanzania na mshambuliaji wa Namungo, Ibrahim Mkoko dhidi ya Mtibwa Sugar. Wakati msimu uliopita mzunguko wa kwanza ilipatikana penalti moja ambayo nahodha wa Simba, John Bocco alikosa katika mechi dhidi ya Biashara United.
Katika mzunguko wa kwanza msimu huu lilipatikana bao la kujifunga mechi ya Mbeya City iliyoshinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji ambayo mchezaji wake Rashid Chambo alijifunga bao la kwanza.
Msimu huu mzunguko wa kwanza timu mbili zilifungwa mabao matatu Geita Gold na Dodoma Jiji wakati uliopita timu zilizofungwa mabao mengi ni KMC na Geita zote mawili mawili.
Msimu uliopita ilipatikana suluhu mechi ya Biashara United dhidi ya Simba na sare kati ya Coastal dhidi ya Azam wakati msimu huu hakuna mechi iliyomalizika na matokeo hayo.
Katika mzunguko wa pili msimu uliopita zilichezwa mechi nane na kufungwa mabao 12 huku michezo miwili kati ya Coastal Union dhidi ya KMC, Mtibwa Sugar na Tanzania Prison ilimalizika bila bao. Msimu huu michezo nane mzunguko wa pili yalifungwa mabao 20 - mara mbili ya msimu uliopita na hakuna mechi ambayo ilimalizika bila kufungwa bao.
Hadi ligi inasimama mzunguko wa pili, Kagera Sugar, Dodoma Jiji na Ihefu ndizo timu pekee ambazo hazikupata ushindi katika michezo miwili wakati huohuo Simba, Yanga na Singida Big Stars ndizo zilizoshinda michezo yote mitatu.
Akizungumzia hali hiyo, mchezaji wa zamani Taifa Stars, Amri Kiemba alisema msimu huu timu nyingi zimefanya maandalizi ya kutosha katika usajili, mbinu na mambo mengine ya kiufundi ndio maana mapema tu mabao mengi yamepatikana.
“Ukiangalia ushindani tu wa michezo ya kwanza ni mkubwa kana kwamba ligi tayari imechanganya na hilo limesababisha hadi matokeo na matukio ya namna hiyo kutokea,” alisema Kiemba na kuongeza:
“Msimu huu timu nyingi zimeimarika katika maeneo ya msingi kiuchumi, mbinu, benchi la ufundi, wachezaji wenye viwango bora tutashuhudia rekodi nyingi.”