Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshambuliaji wa kagera aibuka lulu Ulaya

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Nyota huyo aliondoka Aprili mwaka huu kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu ingawa kiwango anachoendelea kukionyesha kimemfanya kuendelea kusalia humo huku baadhi ya timu mbalimbali zikianza kumnyatia.

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Anuary Jabir aliyeko nchini Ubelgiji kwa ajili ya majaribio kwenye klabu ya KAA Gent huenda akapata dili la kucheza Ulaya msimu ujao kutokana na baadhi ya timu kuhitaji saini yake.

Nyota huyo aliondoka Aprili mwaka huu kwa ajili ya majaribio ya wiki tatu ingawa kiwango anachoendelea kukionyesha kimemfanya kuendelea kusalia humo huku baadhi ya timu mbalimbali zikianza kumnyatia.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud alisema hadi sasa maendeleo ya nyota huyo ni mazuri na kama mambo yataenda vizuri basi huenda akaendelea kusalia huko.

"Kuna timu mbalimbali za Croatia, Uholanzi, Jamhuri ya Czech na Ubelgiji aliyopo ambazo zimeonyesha nia ya dhati ya kumuhitaji kwa ajili ya msimu ujao ingawa mazungumzo nao bado yanaendelea," alisema.

Kwa upande wa Anuary akizungumza na Mwanaspoti kutoka Ubelgiji alisema atahakikisha anaendelea kutumia vizuri nafasi aliyoipata kwani malengo yake ni kuona anacheza kwenye nchi ambazo zimeendelea kisoka.

"Nikiwa kama kijana lazima nionyeshe nina nia ya kufika mbali zaidi ya nilipotoka hivyo naamini licha ya tu ya uwezo wangu na umri nilionao ila ninahitaji kuongeza jitihada ili kufikia malengo yangu," alisema.

Anuary hadi anaondoka Aprili mwaka huu tayari alikuwa ameifungia Kagera Sugar mabao matano ya Ligi Kuu Bara.