Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msemaji Simba aipiga kijembe jezi mpya za Yanga

Msemaji Simba aipiga kijembe jezi mpya za Yanga

Yanga jana usiku imefanya uzinduzi wa jezi zake mpya za aina tatu zitakazo tumika kwa msimu ujao wa 2022/2023 na kumuibua Meneja Habari na mawasiliano wa Simba Ahmed Ally aliyezua  mjadala katika mtandao wa kijamii wa instagram.

Meneja huyo ameandika katika ukurasa wake wa instagram ya kuwa ameshindwa kujizuia kuziongelea jezi hizo kwani hazijamvutia.

"Nimevumilia nimeshindwa acha tu niseme ni mbaya"

Kauli hiyo imeonyesha kiongozi huyo wa Simba ameiponda jezi za watani wake wa jadi na kuongeza kwa kusema;

"Vaa lakini ukijua kuwa umevaa kitu kibaya na ukivaa unanyata"

Aidha Ahmed aliendelea kuitania yanga kwa kusema;

"Sidhani kama KAF(CAF) watakubali 'uniform'  zenye miundombinu maana nimeona mpaka machinjio ya Vingunguti na Dampo la Kinyanwezi"

Licha ya kuzungumza hayo yote meneja huyo aliendelea kusisitiza kuhusu jezi hizo na kuandika; "Ni mbaya mpaka aibu tunaona sisi"

Simba inatarajia kutambulisha jezi zake za msimu 2022/2023 kabla ya Agosti nane.