Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpole arejea kikosini kuivaa Simba

Muktasari:

  • BAADA ya kutokuwa na timu yake ya Geita Gold katika kipindi cha maandalizi ya msimu mpya (Pre Season), mshambuliaji George Mpole amerejea kwenye kikosi cha timu hiyo katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Simba.

BAADA ya kutokuwa na timu yake ya Geita Gold katika kipindi cha maandalizi ya msimu mpya (Pre Season), mshambuliaji George Mpole amerejea kwenye kikosi cha timu hiyo katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Simba.

Mpole aliyeibuka mfungaji bora msimu uliopita akifunga mabao 17, alijiunga na Geita jana jijini Dar es Salaam na kufanya mazoezi ya mwisho kwaajili ya mchezo wa leo ambao ameanza kwenye kikosi cha kwanza.

Uwepo wa Mpole leo unaashiria staa huyo kumalizana na mabosi wake wa Geita Gold tayari kwa kuwatumikia kwa msimu huu.

Wengine walioanza kwenye kikosi cha Geita ni kipa Sebusebu Samson na mabeki Amani Wawa, Yahya Mbegu, Oscar Maasai na Kelvin Yondan.

Viungo ni Kelvin Nashoni, Deusdedith Okoyo na Yusuph Kagoma huku Mpole akiungana na Danny Lyanga na Edmund John katika ushambuliaji.

Benchi wapo Kelvin Kayego, Haruna Shamte, Adeyum Salehe, Hussein Bakari, Ramadhan Chombo, Seleman Ibrahim, Offen Chikola, Raymond Masota na Miraji Athuman.