Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourice Sichone anaisikilizia Chippa United

MOURICE Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Sichone alisema ni kweli ofa hiyo ipo ingawa hadi sasa hajafahamu kinachoendelea.

MSHAMBULIAJI kinda wa Trident FC, Mourice Sichone amesema bado anasikilizia ofa ya Chippa United ya Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sichone alisema ni kweli ofa hiyo ipo ingawa hadi sasa hajafahamu kinachoendelea.

Aliongeza kuwa mazungumzo zaidi yanaendelea kati ya timu hiyo na meneja wake lakini kwa sasa yuko bize na timu yake inayopambana kupanda Ligi Kuu.

“Namalizia mkataba mwezi wa 11 ndio rasmi unaisha, ni kweli kuna wakala walinifuata Afrika Kusini na tukazungumza baadhi ya vitu na ofa yao ilikuwa nzuri,” alisema na kuongeza:

“Kinachoendelea sijafahamu kwa sababu meneja wangu ndio aliendelea kuzungumza nao sasa sijamuuliza imekuwaje na vile niko bize na timu.”

Timu ya nyota huyo Jumamosi ijayo itakamilisha mechi ya mwisho ya ligi Daraja la Kwanza ambayo kama ikishinda itapanda rasmi Ligi Kuu.

Kinda huyo (17) ukiwa msimu wake wa kwanza kukitumikia kikosi hicho amecheza mechi 18 akifunga mabao sita na kutoa asisti nane.