Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yamponza kocha Stars, aaga Afcon

KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars,  Adel Amrouche ni kama ameaga Fainali za Afcon baada ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kumfungia mechi nane kutokana na kauli zake alizozitoa dhidi ya Morocco.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Kamati ya Nidhamu ya Caf, baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Morocco (RMFF), likimlalamikia kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco ina ushawishi ndani ya Caf katika kupanga mechi pamoja na maamuzi.

Kocha huyo aliyeingia Stars mwaka 2023 na kuiongoza kufuzu Fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast, tayari ameiongoza Stars kwenye mechi moja ya fainali hizo dhidi ya Morocco na kufungwa mabao 3-0.

Hiyo inaweza ikawa mechi yake ya mwisho kwa Stars ambayo iko kundi F na Morocco, Congo na Zambia.

Stars imesaliwa na mechi mbili kwenye hatua ya makundi dhidi ya Zambia Januari 21 na DR Congo Januari 24. Hii ina maana mbali na michezo hiyo miwili, Amrouche atakosa michezo mingine minne kama Stars itafika fainali kutokana na idadi ya mechi alizofungiwa.

Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemsimamisha Amrouche kama kocha mkuu wa Stars ambapo Hemed Morocco atakaimu nafasi hiyo akisaidiwa na Juma Mgunda.