Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco awafukuza Mkoko, Lanso kambini kwa utovu wa nidhamu

Muktasari:

  • Katika taarifa iliyotolewa na ZFF, nyota waliofukuzwa ni Ibrahim Mkoko anayekipiga katika klabu ya  Namungo FC na Abdallah Said (Lanso) wa KMC.

Kocha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amewaondoa kambini nyota wake wawili kwa utovu wa nidhamu.

Katika taarifa iliyotolewa na ZFF, nyota waliofukuzwa ni Ibrahim Mkoko anayekipiga katika klabu ya  Namungo FC na Abdallah Said (Lanso) wa KMC.

Utovu wao wa nidhamu uliotajwa katika taarifa hiyo ni kuchelewa kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mashindano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Januati 3, 2025 msimu huu yakihusisha timu za Taifa, ikiwa tayari walisharuhusiwa na klabu zao.

Aidha, Morocco amemuongeza Ali Juma Maarifs (Mabata) anayekipiga kwenye kikosi chA Uhamiaji inayoshiriki Ligi kuu Zanzibar.

Heroes iliingia kambini Desemba 24 na jana ilianza rasmi maandalizi.