Mnoga, Starkie waanza Taifa Stars

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ ametoa kikosi kitakachoanza kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Afrika ya Kati huku akiwaanzisha makinda wawili Haji Mnoga na Ben Starkie wote wenye umri wa miaka 19.
Starkie ni kiungo mshambuliaji anayeichezea Spalding ya England na Mnoga ni beki wa kulia anayekipiga Weimouth ya England pia hii ni mara yao ya kwanza kuichezea Taifa Stars.
Katika kikosi hicho, kocha Kim golini amemuanzisha Metacha Mnata huku mabeki wakiwa Mnoga, Nickson Kibabage, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.
Viungo ni Novatus Dismas, Starkie, na Feisal Salum ‘Feitoto’ huku washambuliaji wakiwa ni Abdillahie Yusuph, Mbwana Samatta na Kelvin John.
Katika benchi wapo, Aboutwalib Msheri,Aishi Manula, Lusajo Mwaikenda, Farid Mussa, George Mpole, Saimon Msuva, Zawadi Mauya, Joshua Mwakasaba, Tepsi Evance, Aziz Andambile na Reliants Lusajo.
Mechi hiyo iliyo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ni maandalizi kwa Taifa Stars inayojipanga na michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) na fainali za mataifa ya Afrika (AFCON).