Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tausi Royals haishikiki WBDL

TAUSI Pict

Muktasari:

  • Huu ni mwaka wa pili kwa timu hiyo kushiriki ligi hiyo na imeongoza kwa kufunga pointi 666 katika michezo saba iliyocheza, huku JKT Stars ikifunga pointi 563.

Tausi Royals haishikiki katika Ligi ya kikapu Dar es Salaam (WBDL) na inaongoza kwenye msimamo ikiwa na pointi 14 ikifuatiwa na JKT Stars yenye 13.

Huu ni mwaka wa pili kwa timu hiyo kushiriki ligi hiyo na imeongoza kwa kufunga pointi 666 katika michezo saba iliyocheza, huku JKT Stars ikifunga pointi 563.

Takwimu ya msimamo iliyotolewa na kamishna wa ufundi na mashindano wa Ligi ya BDL, Haleluya Kavalambi, imeonyesha DB Lioness inashika nafasi ya tatu kwa pointi 13.

Zinazofuatia ni Jeshi Stars pointi 12, DB Troncatti 12, Twalipo Queens 12, Polisi Stars 11, Vijana Queens 10, Pazi Queens 10,  Reel Dream tisa.

Zingine ni Kigamboni Queens tisa, Kurasini Divas tisa, City Queens nane, UDSM Queens nane,  Mgulani Stars saba na Ukonga Queens nane Msimamo (Wanawake).