Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize ana akili ya kizungu kimtindo

MZIZE Pict

Muktasari:

  • Sisemi kama ni wote ila wengi wao wanaziona timu ambazo zimewapa fursa tangu wakiwa vijana wadogo kama sehemu ya maisha yao hivyo hujitahidi kuishi nazo vizuri ili wasiondoke au kumaliza maisha ya soka vibaya ndani ya timu hizo.

WACHEZAJI wa kizungu huwa wanazipa heshima na kuzithamini sana timu ambazo zimewapa fursa ya kujitangaza na kuingia katika daraja la juu kiushindani.

Sisemi kama ni wote ila wengi wao wanaziona timu ambazo zimewapa fursa tangu wakiwa vijana wadogo kama sehemu ya maisha yao hivyo hujitahidi kuishi nazo vizuri ili wasiondoke au kumaliza maisha ya soka vibaya ndani ya timu hizo.

Kijiwe kina kumbukumbu ya baadhi ya mastaa wa soka duniani ambao waliamua hata kutojiunga na timu nyingine zilizowahitaji na kuamua wabakie katika timu zilizowakuza tangu utotoni hadi walipofikia katika levo ya juu.

Lakini hili huwa ni nadra kwa wachezaji wengi wa Kiafrika kwa sababu huwa kwao kipaumbele cha kwanza ni fedha wanapoiona mezani wanajikuta wanasahau mambo ya kutoa kipaumbele kwa klabu zilizowaibua au kuwalea hadi wamefika mahali walipo.

Tumekumbushana hilo hapa kijiweni kwetu baada ya kusikia Yanga inajiandaa kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka Zamalek ya Misri kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Clement Mzize ambaye ameonyesha kiwango bora msimu huu.

Kama Mzize angekuwa na mawazo ya kutanguliza masilahi yake binafsi mbele, leo hii Yanga isingekaribia mamilioni ya fedha kupitia mauzo ya mchezaji huyo kwani mwishoni mwa msimu wa 2023/2024 mkataba wake wa awali ulifikia tamati na angeweza kuondoka bure kama mchezaji huru.

Kwa vile kulikuwa na ofa nyingi mezani, maana yake fungu la usajili angeweka lote mfukoni mwake bila Yanga kupata chochote kwani hakuwa tena mali yao.

Hata hivyo, Mzize alikumbuka kuwa Yanga ndio timu iliyomtoa katika mazingira magumu kisha ikamuamini na kumpa nafasi ya kuonyesha kipawa chake ambacho leo kimempa jina kubwa ndani na nje ya Tanzania.

Akakubali kuongeza mkataba ili hata akiuzwa, klabu hiyo ipate fedha kuliko angeondoka bure na hiyo yote inachangiwa na heshima kwa namna timu hiyo ilivyomfungulia dunia.