Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmorocco wa Azam na kipimo cha Pamba

Muktasari:

  • Azam itaikaribisha Pamba kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku mara baada ya Nyuki wa Tabora kumalizana na maafande wa Prisons ikiwa ni moja ya mechi mbili zinazopigwa leo katika ligi hiyo iliyopo raundi ya tatu.

KOCHA Mkuu mpya wa Azam FC, Rachid Taoussi kwa mara ya kwanza leo Jumamosi anatarajiwa kutupa karata katika mechi ya Ligi Kuu Bara wakati atakapokiongoza kikosi hicho dhidi ya Pamba Jiji, huku Tabora United ikiwa nyumbani itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Azam itaikaribisha Pamba kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuanzia saa 1:00 usiku mara baada ya Nyuki wa Tabora kumalizana na maafande wa Prisons ikiwa ni moja ya mechi mbili zinazopigwa leo katika ligi hiyo iliyopo raundi ya tatu.

Ni mechi ya aina yake inayozikutanisha timu ambazo zimeanza msimu kwa kusuasua, Azam ikitoka suluhu na JKT Tanzania, huku Pamba ilianza kwa suluhu mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Prisons na Dodoma Jiji.

Haitakuwa mechi nyepesi kwa timu zote, lakini utamu ni zinakutana timu zisizofahamiana na hata makocha hao hawajuani kivile, kwani Goran ni mzoefu wa Ligi ya Bara akianzia kuinoa Simba kisha Tabora United aliyokuwa nayo msimu uliopita.


REKODI ZAO

Azam na Pamba Jiji zimekutana mara mbili katika mashindano tofauti, kwa mara ya kwanza ilicheza katika michuano ya FA mwaka 2019 na Matajiri wa Chamazi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, huku mabao yote yakifungwa na Ramadhani Singano ‘Messi’.

Mchezo wa pili Pamba ilikuwa nyumbani, ikikaribisha Azam katika mchezo wa kirafiki Mwaka 2022 na Matajiri hao kurudia rekodi yake ya kuichapa mabao 2-0 tena, hii ikiwa na maana leo kuna kazi kwa Pamba kutaka kufuta unyonge kwa Azam, lakini kila moja ikisaka pointi tatu za kwanza za Ligi Kuu.

Pamba itaendelea kuwategemea washambuliaji wapya waliosajiliwa msimu huu, akiwamo George Mpole, Eric Okutu na Ben Nakibinge, James Mwashinga ambao bado hawajaonyesha makali, japo kocha Goran alisema anaamini mbele ya Azam moto utawaka leo, huku ikijivunia kipa Yona Amos aliyekuwa na timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza mechi mbili za kuwania tiketi ya Afcon 2025.

Kwa upande wa Azam inatambia mastaa kama Feisal Salum ‘Fei Toto’, Gibril Sillah, Jhonier Blanco na wengine ambao watapenda kujitofautisha chini ya kocha Taoussi na biokla shaka Pamba watakuwa na kibarua kigumu Chamazi.

Kocha wa Pamba, Goran Kaponovic alisema mechi haitakuwa rahisi kwa upande wao kwani wapinzani wanakocha mpya ambaye mbinu zake hazijulikani.

Aidha alieleza kuwa, wachezaji wa Azam FC watajituma sana kuhakikisha wanaonyesha viwango vyao kwa kocha mpya ili waweze kupata namba.

“Nimefanyia kazi eneo la ushambuliaji ambalo lilikuwa changamoto katika kikosi changu, hivyo natarajia makubwa katika mechi hii.

Wapinzani wetu wanauzoefu kutuzidi lakini mpira wa miguu unahitaji juhudi ili kufanikisha malengo ya timu, hivyo naamini tunaweza kufanya vizuri,” alisema Goran.