Mkwabi amchukulia fomu Karia

Friday June 11 2021
mkwabi pic
By Thomas Ng'itu

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Swedi Mkwabi leo mchana amemchukulia fomu ya kugombea urais, Wallace Karia katika makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF)

Mkwabi alifika katika ofisi hiyo saa 8:30 mchana akiwa na gari lake aina ya BMW X5  na moja kwa moja aliingia katika ofisi hizo kwenda kuchukua fomu.

Uwepo wake katika ofisi hizo ulizua maswali mengi kwani haikujikana moja kwa moja kama ni yeye ndiye amekuja kuchukua fomu au amekuja kumchukulia mtu.

Alipotoka baada ya takribani dakika tano, Mkwabi amesema alifika katika ofisi hizo kwa lengo la kumchukulia fomu Wallace Karia.

“Karia yupo kanda ya ziwa katika shughuli za Shirikisho kwahiyo mimi kama mdau nimekuja kumchukulia fomu ili aendelee kuongoza," alisema Mkwabi.

Uchaguzi wa TFF unatarajia kufanyika mkoaniTanga tarehe Agosti 7 mwaka huu.

Advertisement

TFF imesema wengine waliochukua fomu hadi sasa ni Evans Mgeusa na Zahor Mohammed Haji huku shughuli ya uchukuaji na urudishaji itafungwa rasmi Juni 12.

Advertisement