Mkosa aongoza kwa ufungaji

Muktasari:
- Katika chati za wafungaji vinara wa msimu huu kufikia sasa, Mkosa anafuatiwa na Jonas Mushi kutoka JKT aliyefunga pointi 455, kisha yupo Tyrone Edward wa timu ya UDSM Outsiders anayeshika nafasi ya tatu kwa kufunga pointi 445.
KUKIWA kumesaliwa na mechi za raundi tatu kabla ya kukamilisha michezo 30 ya mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), mchezaji Amin Mkosa wa timu ya Mchenga Stars anaongoza kwa kufunga pointi 488.
Katika chati za wafungaji vinara wa msimu huu kufikia sasa, Mkosa anafuatiwa na Jonas Mushi kutoka JKT aliyefunga pointi 455, kisha yupo Tyrone Edward wa timu ya UDSM Outsiders anayeshika nafasi ya tatu kwa kufunga pointi 445.
Wachezaji ni Stanley Mtunguja (Ukonga Kings) pointi 442, Fotius Ngaiza (Vijana) 386, na Jamel Marbuary (Dar City) 375.
Wengine ni Alfan Mustafa (Vijana) 359, Isaya William (DB Oratory) 349, Enerco Maengera (ABC) 343 na Victor Michael (Vijana) 335.
Kwa upande wa ufungaji wa maeneo ya mitupo ya pointi tatu (three pointers), anayeongoza ni Jonas Mushi (JKT) aliyefunga ‘three points’ mara 66 akifuatiwa na Abdul Kakwaya (DB Oratory) aliyefunga mara 62.
Wachezaji wengine ni Sam Agutu (Mchenga Stars) mara 58, Oscar Mwituka (Savio) mara 54, Jamel Marbuary (Dar City) mara 54, Emanuel Kibona (KIUT) mara 52 na Felix Luhamba (JKT) mara 48.