Mitambo ya fedha wamo Chama, Maxi

NI ligi mbili pekee ambazo hazijaanza kuchezwa hadi sasa nchini, First League na Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), lakini Ligi Kuu Bara na ile ya Championship tayari zimeanza na kwa sasa zikiwa katika raundi ya tatu kila moja.
Ligi hizo zilianza wakati dirisha la usajili likiwa wazi kabla ya kufungwa rasmi Agosti 31 na kwa hesabu za haraka zilizofanywa na Mwanaspoti kupitia usajili huo ni kwamba msimu huu jumla ya wageni 185 ambao ni wachezaji, wataalamu wa benchi la ufundi na utawala kutoka nje ya Tanzania wamekula shavu.
Usajili huo ni kwa ligi zote nne ambazo zipo chini ya Bodi la Ligi (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na rekodi zinaonyesha kwa Ligi Kuu kuna wageni 127, WPL (48), Championship ina 10 huku First League ikiwa hakuna timu iliyoajiri mgeni hata mmoja.
Hii ni tofauti na msimu uliopita ambapo katika Ligi Kuu kulikuwa na wageni 111, WPL (38), Championship (21) na First League (5) na kufanya kuwa na jumla ya wageni 175.
Wafanyakazi wote hao wanapaswa kulipiwa vibali kutoka mamlaka tatu, Idara la Uhamiaji inayotoa kibali cha makazi, Wizara ya Kazi na Ajira inayotoa vibali vya kazi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambao hutoa leseni kwa wachezaji isipokuwa makocha na waajiriwa wengine ambao sio wachezaji.
Vibali vinavyotolea na Idara ya Uhamiaji kwa nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi hulipwa Dola 500 kwa mtu mmoja, wale wengine wote kutoka nchi za SADC na Ulaya wanatakiwa kulipa Dola 2000 kwa mtu mmoja.
Wizara ya Kazi na Ajira hulipwa dola 1000 kwa wote wakati TFF kila mchezaji bila kujali nchi anayotoka analipa Sh 4 milioni isipokuwa makocha na waajiriwa wengine ambao sio wachezaji.
Ligi Kuu Bara msimu huu ina jumla ya wachezaji 95 na wataalamu wa benchi la ufundi pamoja na viongozi ni 30 kutoka timu 13 kati ya 16 zinazoshiriki ligi hiyo jumla ikiwa ni 127 ambao ni wageni.
Ligi ya wanawake ina wachezaji 48 wakati Championship ina 10 kutoka nje huku First League yenyewe haina hata mmo. Hivyo kwa ujumla wake wanamichezo wote kwenye soka wapo 185. Kati ya hao 185 wachezaji na makocha wanaotoka mabara matatu ya Afrika wakiwamo wanaotoka nchi za SADC, Afrika Magharibi, Kusini, Kaskazini, Kati na Ulaya jumla yake wapo 119 wakati Afrika Mashariki ni 66.
Ikumbukwe kwamba benchi la ufundi na mabosi wengine wao wanalipa ada ya makazi (Idara ya Uhamiaji) na kibali cha kazi (wizara ya Kazi na Ajira) ila TFF hawalipi.
Jumla ya pesa inayopatika kwa wafanyakazi wote wa kigeni (wachezaji, makocha na viongozi) kutoka TFF, Uhamiaji na Wizara ya Kazi ni zaidi ya Sh 1.7 bilioni kwa mwaka.
TFF yenyewe huingiza zaidi ya Sh 600 milioni (36%) kutokana na ada za wachezaji, Uhamiaji ni zaidi ya Sh 640 milioni (38%) malipo ya vibali vya makazi kwa wageni wote na Wizara ya Kazi na Ajira zaidi ya Sh 400 milioni (26%).
Hata hivyo, Ligi Kuu ndio hupata pesa nyingi zaidi kwani kati ya hizo huingiza zaidi ya Sh 1.2 bilioni (70%), WPL zaidi ya Sh 408 milioni (24%) na Championship ni zaidi ya Sh 105 milioni (6%).
Timu tano za Ligi Kuu ndizo hulipa zaidi ukilinganisha na nyingine ambazo zimeajiri wachezaji na makocha wa kigeni kwani hulipa zaidi ya Sh 787 milioni sawa na 47%.
Simba na Azam FC ndizo zinaongoza kwa kulipa pesa nyingi kuliko nyingine, timu hizo hulipa zaidi ya Sh 170 milioni (10%) kila timu ikifuatiwa na Yanga zaidi ya Sh 156 milioni (9%), Singida Big Stars zaidi ya Sh 148 milioni (9%) na Tabora United zaidi ya Sh 141 milioni (8%).
SIMBA - 18
Wachezaji ni 12; Kouame Kramo (Ivory Cost), Clatous Chama (Zambia), Junior Che Malone na Willy Onana (Cameroon), Moses Phiri (Zambia), Jean Baleke (DR Congo)
Sadio Kanoute (Mali), Said Ntibazonkiza (Burundi), Luis Miquissone (Msumbuji), Ayoub Lakred (Moroco), Henock Inonga na Fabrice Ngoma (DR Congo)
Wataalamu wa benchi la ufundi ni sita; Roberto Oliveira ‘Robertinho’-Kocha Mkuu, Ouanane Sellami-Kocha Msaidizi,
Mikael Igendia-Meneja wa timu na Mkuu wa Sayansi ya Michezo, Corneille Hategekimana-Kocha wa Viungo, Daniel Cadena-Kocha wa Makipa na Wycliff Omom-Mtaalamu wa Tiba ya Viungo.
AZAM FC -17
Upande wa wachezaji wapo 12; Cheikh Sidibe (Senegal), Gibril Sillah (Gambia), Iddrisu Abdulai (Ghana), Kipre Zunon (Ivory Coast), James Akaminko (Ghana), Ali Ahamada (Ufaransa), Malickou Ndoye (Senegal).
Wengine ni Daniel Amoah (Ghana), Alassane Diao (Senegal), Yannick Bangala (DR Congo), Idris Mbombo (DR Congo) na Prince Dube (Zimbabwe).
Benchi la Ufundi wapo watano ambao ni Youssouph Dabo-Kocha Mkuu (Senegal), Bruno Ferry-Kocha Msaidizi (Ufaransa), Khalifa Ababakar Fall-Kocha wa Makipa (Senegal), Ibrahim Diop-Mchambuzi wa Mechi (video analyst) na Jean-Laurent Geronimi- Mtaalamu wa Mazoezi ya viungo (Ufaransa)
SINGIDA BIG STARS -17
Wachezaji ni 12; Nicholas Gyan (Ghana), Bruno Gomes (Brazil), Kazadi Francy (DR Congo), Carno Ngeyikwela Beimesi (DR Congo), Joash Onyango (Kenya), Nico Wadada (Uganda)
Morice Chukwu (Nigeria), Enock Agyei (Ghana), Duke Abuya (Kenya), Marouf Tchakei (Togo), Meddie Kagere (Rwanda) na Elvis Rupia (Kenya).
Benchi la ufundi ni watano; Thabo Senong-Kocha Msaidizi, Thembalethu Moses-Kocha wa Makipa, Kelvin Mandla-Kocha wa Viungo, Mathias Lule-Kocha Msaidizi (Uganda) na Ramadhan Nswanzurimo-Mkurugenzi wa Ufundi (Burundi).
YANGA - 16
Wachezaji 12; Max Nzengeli (DR Congo), Fred Gift (Uganda), Khalid Aucho (Uganda), Kennedy Musonda (Zambia), Djui Diarra (Mali), Kouassi Yao (Ivory Cost), Joyce Lomalisa (DR Congo), Aziz KI (Ivory Cost), Jesus Moloko (DR Congo), Mahlatse Makudubela (Afrika Kusini), Pacome Zouzoua (Ivory Cost) na Hafiz Konkoni (Ghana).
Benchi la Ufundi na Utawala ni watano; Miguel Gamondi-Kocha Mkuu (Argentina), Moussa N’Daw-Kocha Msaidizi (Senegal), Taibi Lagrouni-Kocha wa mazoezi ya viungo (Moroco), Alaa El Meskini-Kocha wa Makipa (Morocco) na Mtendaji Mkuu Andrew Mtine (Zambia).
TABORA UNITED -14
Wachezaji 12; John Nakibinge (Uganda), Noble John (Nigeria), Pemba Kingu (DR Congo), Lulihoshi Heritier (DR Congo), Eric Okotu (Ghana), Papy Tshishimbi (DR Congo), Jean Touya (Burundi), Jackson Mbombo (DR Congo), Andy Bikoko (DR Congo), Lumiere Banza (DR Congo), Paulin Kasindi (DR Congo)
Ngonyani Mutuale (DR Congo).
Wakati benchi la ufundi ni wawili; Goran Kopunovic -kocha mkuu (Serbia) na Razack Siwa- kocha wa makipa (Kenya)
COASTAL UNION -11
Wachezaji wapo 10; Justine Ndikumana (Burundi), Dennis Modzaka (Ghana), Henock Mayala (DR Congo), Shadreck Mulingwe (Zambia), Felly Mulumba (DR Congo), Yakubu Salah (Nigeria), Ley Matampa (DR Congo), Konare Malienne (Mali), Fran Golubic (Croatia) na Roland Beakou (Benin)
Kwenye benchi la ufundi yupo mmoja kocha mkuu, Mwinyi Zahera - DR Congo.
KAGERA SUGAR -8
Wachezaji wapo nane; Stephen Duah (Ghana), Deus Bukenya (Uganda), Hamis Kizza (Uganda), Obrey Chirwa (Zambia), Appolinaire Tientcheu (Cameroon), Dissan Galiwango (Uganda), Nicholas Kasozi (Uganda) na Ngeleka Katembua (DR Congo)
NAMUNGO FC - 8
Ina wachezaji sita; Sedjro Counou (Benin), Baba-Seidou Blandja (Togo), Christopher Okoje (Kenya), Jonathan Nahimana (Burundi), Fabrice Ngoy (DR Congo) na Derick Mukombozi (Burundi).
Benchi la ufundi wawili; Cedric Kaze -kocha mkuu na kocha wa makipa Vladimir Niyonkuru wote kutoka Burundi.
KMC -4
Wachezaji watatu; Isah Aliyu (Nigeria), Ibrahim Ahmed (Kenya) na Abdikarim Mahamoud (Somalia) pamoja na kocha mkuu, Abdulhamid Moalin (Somalia).
DODOMA JIJI - 4
Wachezaji watatu; Mwana Kibuta (DR Congo), Christian Zigah (Ghana) na Joseph Zziwa (Uganda) huku benchi la ufundi likiwa na kocha mkuu pekee, Melis Medo (Marekani).
IHEFU FC -3
Wapo watatu; Never Tigere (Zimbabwe), Moubarack Amza (Cameroon) na Victor Akpan (Nigeria).
TANZANIA PRISONS -3
Ni wachezaji watatu pekee; Joshua Otieno (Kenya), Mambote Batshi Assis (DR Congo) na Messi Atangana (Cameroon)
GEITA GOLD -1
Hii ina mchezaji mmoja kutoka Uganda, Hassan Mahamud (Uganda) wakati JKT Tanzania, Mashujaa FC na Mtibwa Sugar zenyewe hazijaajiri mchezaji wala kiongozi yeyote wa kigeni.
CHAMPIONSHIP JUMLA 10
Upande wa timu zinazoshiriki Ligi ya Championship timu timu mbili pekee zenye wachezaji wa kigeni ambao jumla yao ni 10.
Ken Gold imesajili nyota nane wa kigeni; Victor Odinkwazuka (Nigeria), Amukena Lubinda (Zambia), Danton Mumba (DR Congo), Emmanuel Ngama (Burundi), Paul Kambulo (DR Congo), Damilare Clement (Nigeria), Samson Dauda (Nigeria) na Kenneth Chama (Zambia)
Biashara United imesajili wawili; Inocent Edwin (Nigeria) na Boban Bogere Zirintusa (Uganda).
Mbeya City, Mbeya Kwanza, Pamba FC, Pan African, Ruvu Shooting, Polisi Tanzania, Copco, Stand United, Fountain Gate FC, TMA Stars, Transit Camp, Cosmopolitan, Green Worrios na Mbuni FC zenyewe hazina mchezaji wa kigeni.
LIGI KUU WANAWAKE (WPL) - 47
Kwenye ligi hii ya WPL, ni timu mbili pekee ambazo hazijasajili mchezaji hata mmoja wa kigeni ambao ni Mabingwa watetezi JKT Queens na Amani Queens.
SIMBA QUEENS -12
Vivian Corazone (Kenya), Asha Djafari (Burundi), Baraka Olaiya (Nigeria), Danai Bhobho (Zimbabwe), Joelle Bukuru (Burundi),
Carolyne Rufa (Kenya), Joanitah Ainembabazi (Uganda), Ruth Ingosi (Kenya), Daniela Ngoyi (DR Congo), Isabelle Diakiese (DR Congo), Nabbosa Ritticia (Uganda) na Elizabeth Mutukiza (Kenya).
FOUNTAIN PRINCESS - 10
Wachezaji 10; Winfrida Ouko (Kenya), Chebeti Monicah Odato (Kenya), Myline Awuor (Kenya), Inviolata Mukoshi (Kenya), Nabbosa Ritticia (Uganda), Priviledge Mupeti (Zimbabwe), Aniella Uwimana (Burundi), Topister Nfaula Situma (Kenya), Suzanne Zilfa (Burundi) na Annonciate Nshimirimana (Burundi)
YANGA PRINCESS - 10
Wachezaji tisa; Safiatu Salifu (Ghana), Wincate Kinyua (Kenya), Marry Saiki (Nigeria), Diana Antwi (Ghana), Precious Christopher (Nigeria), Adejoke Busirat (Ghana), Faiza Seidu (Ghana), Richanelle Kiteko (DR Congo) na Numpoa Traore (Burkina Faso).
Kocha mkuu wa timu hiyo ametoka Zambia, Haaalubono Charles.
CEASIAA QUEENS FC -7
Wachezaji ni Joanitor Naggayi (Uganda), Sheeba Zalwango (Uganda), Stella Musibika (Uganda), Nagadya Naume (Uganda), Bernadette Namwenge (Uganda), Resty Nanziri (Uganda) na Adelaide Nimfasha (Burundi).
BUNDA QUEENS-5
Nyota hao ni Saumu Baya (Kenya), Fidu Mwahaga (Kenya), Hannah Njoroge (Kenya), Sylivia Otieno (Kenya) na Faida Habimana (Burundi)
ALLIANCE GIRLS - 3
Wasajiliwa watatu; Anita Adongo Agunda, Linda Nasimiyu Kihara na Nelly Kache Jonathan wote kutoka Kenya.
GEITA QUEENS -I
Hii imepanda msimu huu imesajili mmoja kutoka Kenya, Florida Omusanga pamoja na Baobab Queens nao wana mmoja Jeanne Pauline (Rwanda).
FIRST LEAGUE -0
Zamani ilijulikana kama Ligi Daraja la Pili sasa ni First League ambayo ina timu 16, hakuna timu iliyosajili mchezaji wa kigeni, timu hizo ni;
African Lyon, Alliance FC, Dar City FC, Kasulu United, Kiluvya FC, Kurugenzi FC, Malimao FC, Mwadui FC, Mapinduzi FC, Nyumbu FC, Tanesco SC, TRA Kilimanjaro FC na Tunduru Korosho.