Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mitambo ya fedha

Muktasari:

Klabu nyingi ziko kwenye maaandalizi ya mwisho kwa ajili ya ligi kuanza huku majina mapya kwa baadhi ya klabu yakiwa kivutio kwa wengi na iwapo klabu zote 16 zitadhamiria, basi zinaweza kuwatumia baadhi ya wachezaji wake kufanya biashara nzuri itakayowaingiza fedha nyingi.

SOKA ni biashara na biashara siku zote ni matangazo. Dirisha la usajili Tanzania Bara limefungwa rasmi juzi Alhamisi usiku, huku baadhi ya klabu zikihitimisha kwa kusajili nyota mbalimbali wenye majina makubwa. Hata hivyo, mashabiki wa soka wanangoja kuona makali ya nyota hao mara Ligi Kuu Tanzania Bara itakapoanza mikikimikiki yake.

Klabu nyingi ziko kwenye maaandalizi ya mwisho kwa ajili ya ligi kuanza huku majina mapya kwa baadhi ya klabu yakiwa kivutio kwa wengi na iwapo klabu zote 16 zitadhamiria, basi zinaweza kuwatumia baadhi ya wachezaji wake kufanya biashara nzuri itakayowaingiza fedha nyingi.

Achana na sura zao kwenye matangazo, lakini hata mauzo ya jezi na vifaa vingine vinaweza kutumika kuzitajirisha klabu hizo kama ambayo klabu za Ulaya zinazvyofanya.

Klabu zinaweza kuwataumia mastaa hao kujenga mazingira ya kuwavutia wafadhili na wadhamini na hatimaye zile shida ndogondogo zinaweza kuyeyuka katika klabu hizo kwa kuvuna mapato ya kutosha.

Mwanaspoti limewatathimini nyota waliosajiliwa na waliopo katika klabu mbalimbali za Ligi Kuu kama wakitumiwa vyema na klabu hizo wanaweza kuzinufaisha kimapato kwani klabu zinaweza kupiga pesa nzuri kibiashara tofauti na ilivyozoeleka.

 

Andrey Coutinho, Yanga

Kiungo mshambuliaji, huyu ni Mbrazili anayekipiga Yanga, ni mmoja wa wachezaji anayependwa zaidi Yanga na mashabiki na hata wazee wa klabu hiyo kutokana na uwezo wake wa kusakata soka la kuvutia. Mchezaji huyo ni mahiri kwenye kupiga faulo, mashuti na hata kucheza kwa mbinu mbalimbali za kuvutia. Licha ya kwamba hapati nafasi mara kwa mara, winga huyo anabaki kuwa kipenzi cha mashabiki na endapo klabu itamtumia vizuri kwa kumpa kipaumbele kwenye matangazo ya kibiashara au kumhusisha kwenye uuzaji wa jezi za klabu ni wazi kuwa Yanga itaweza kupiga fedha.

Mbali na mchezaji huyo, Yanga inaye kiungo mchezeshaji mwingine, Haruna Niyonzima ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Rwanda, ni mchezaji anayetambulika kote Afrika Mashariki na ni mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kucheza soka la kuvutia. Uwezo wake unamuuza na kama Yanga ikimtumia vizuri itafaidika. Wengine wanaoweza kuizalishia Yanga fedha ni Simon Msuva, Amissi Tambwe na hata nyota wake wapya wa kigeni Donald Ngoma na Vincent Bossuo.

 

Mussa Hassan ‘Mgosi’ (Simba)

Kwa sasa kama ukisafiri au ukienda mazoezi ya Simba, mashabiki wengi huwa wanataja jina la Mgosi, hii ni kuonyesha namna gani straika huyo anavyokubalika zaidi Simba. Kiashiria kimoja ni kukabidhiwa kwake unahodha baada ya kusajiliwa Simba. Mgosi ataweza kutumika vizuri na Simba na ubora wake na upambanaji wake kwenye klabu mbalimbali alizocheza umekuwa ukimpa umaarufu ambao kibiashara unaweza kuinufaisha Simba.

Straika Ibrahim Ajibu anafuata nyayo hizo hizo. Amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu na hata kuwapa furaha Wanasimba wakati ule wa hali inapokuwa mbaya. Ajibu tayari ni staa na ni mchezaji anayekubalika na anaweza kuisaidia Simba kibiashara. Pia, Simba ina wachezaji kama Hassan Is’haka, Said Ndemla, Hamis Kiiza na hata Jonas Mkude aliyewahi kuuza sura katika tangazo la magodoro.

 

Juma Kaseja (Mbeya City)

Kipa Mpya wa Mbeya City, Juma Kaseja bado anatajwa kuwa kipa bora wa Tanzania, licha ya kuwa hajacheza soka la kishindani kwa kipindi kirefu.

Kaseja ni kipa mahiri na ambaye amekuwa na sifa kubwa ndani na nje ya nchi kutokana na umahiri wake. Amekuwa akifanya biashara ya matangazo na makampuni mbalimbali Tanzania yakiwemo Benki ya DTB, Pepsi na mengine, hivyo ni wakati wa Mbeya City kumtumia kukuza mashabiki na kutafuta wadhamini.

Mchezaji mwingine anayekubalika Mbeya City ni Mwagane Yeya ambaye hata hivyo ametemwa, ila kama angetumiwa vizuri angeweza kuinufaisha kwani mmoja wa wachezaji waliocheza kwa mafanikio kwenye klabu hiyo na cha ziada ni mwalimu wa shule ambaye amekuwa akipendwa na wanafunzi.

 

Pascal Wawa (Azam)

Beki Muivory Coast wa Azam, Pascal Wawa amepata umaarufu mkubwa kupitia Ligi Kuu msimu uliopita, lakini zaidi kwenye Kombe la Kagame la mwaka huu ambapo aliiwezesha Azam kutwaa ubingwa bila ya kuruhusu lango lake kufungwa.

Wawa aliyepachikwa jina ‘Waziri wa Ulinzi’ ni sura mpya ya kuitangaza Azam. Kama Azam imedhamiria kuuza jezi na vifaa vingine vya kimichezo, basi Wawa ni mtu sahihi wa kumtumia kutokana na kuwa kivutio kwa wengi. Wawa ni mahiri kwenye kukaba na kupandisha mashambulizi.

Mbali na Wawa yuko nahodha wa timu hiyo, John Bocco ambaye amekuwa akitumika kwenye matangazo mbalimbali ya kibiashara. Kimsingi Bocco ni mfungaji bora na mchezaji mwenye mafanikio makubwa zaidi kuliko wachezaji wote waliichezea Azam. Bocco ndiye aliyepambana kuifanya Azam inakuwa ilipo sasa na hii imekuwa ikimpa heshima na kumfanya kuwa mchezaji wa kipekee. Azam inahitaji kuendelea kumtumia kuuza na kutangaza timu kupitia kwake.

 

Hamad Ndikumana (Stand United)

Beki Hamad Ndikumana ni mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya, tayari amejiunga na Stand na atakuwa akikipiga sambamba na wachezaji wengine wapya kama Amri Kiemba.

Selemani Kassim ‘Selembe’ na wengine kibao. Umaarufu wa msanii wa Uwoya utaweza kutumiwa na Stand United kwa kumtangaza Ndikumana kwenye vyombo vya habari na kumhusisha na msanii huyo ili kuwavutia wadau na hata timu kuweza kujiingizia fedha. Stand inaweza kwenda mbali na kumtumia Uwoya kujitangaza licha ya kuwa itakuwa na Ndikumana ambaye ni beki mzoefu na imara.

Stand pia itakuwa na fursa ya kutumia umaarufu wa Nahodha, Haroun Chanongo aliyejikusanyia umaarufu akiwa Simba na kuwa moja ya wachezaji watakaotumika kuuza jezi na bidhaa nyingine pamoja na kuvutia wawekezaji mbalimbali wa kuidhamini timu.

 

Nizar Khalfan (Mwadui)

Kiungo mchezeshaji wa Mwadui, Nizar Khalfani ni miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye kikosi cha Mwadui kutokana na umahiri wake, lakini pia ubora wake wa kupiga pasi.

Nizar ni kiungo ambaye amekuwa akitawala vyema safu ya kiungo na amewahi kutamba akiwa na Yanga, Mtibwa Sugar na Moro United.

Pia aliwahi kuichezea Vancouver Whitecaps ya Canada. Nizar ni mchezaji ambaye anaweza kutumika na klabu ya Mwadui kuitanganza timu kwa kuzungumza na vyombo vya habari na hata kuweza kuwa kivutio cha biashara. Wengine ni Athumani Chuji ambaye ni kiungo maarufu, pia yuko kipa Shaaban Kado.

 

Wengine

Wachezaji wengine ni Beki George Kavilla (Kagera Sugar), Nahodha Erick Ngwegwe na kiungo Abdallah Seseme (Toto African), straika Fully Maganga na winga Mohamed Samatta (JKT Mgambo). Pia, Samuel Kamuntu na Saady Kipanga (JKT Ruvu), kipa Hussein Sharrif ‘Casillas’ na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), Edo Christopher (Toto Africans), Atupele Green wa Ndanda, William Lucian ‘Gallas’ja na Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ na Migeria Abaslim Chidiebele (Coastal Union).