Mirambo: Uturuki kumetupa fundisho kubwa

Muktasari:
- Serengeti Boys imepangwa Kundi A, pamoja na timu za Nigeria, Angola na Uganda huku B, likiwa na Guinea, Cameroon, Morocco na Senegar
Dar es Salaam. Kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys', Oscar Mirambo amesema mechi walizocheza Uturuki za kwenye michuano ya Uefa Assist zitawapa matokeo mazuri katika mashindano ya AFCON yatakayopigwa hapa nchini.
Serengeti Boys ilicheza mechi tatu, wameambulia ushindi wa mchezo mmoja tu walipoifunga Australia bao 3-2 kisha wakapoteza kwa wenyeji Uturuki kwa mabao 5-0 na Guinea walianza kuwachapa kwenye mechi ya ufunguzi kwa bao 1-0.
Mirambo amesema mechi hizo zimewafaidisha kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwajua wapinzani wao kwenye AFCON.
"Ukiachana na wapinzani wetu ambao kwa sasa hawatakuwa wageni kwetu, vijana wamepata uzoefu wa kucheza mechi za kimataifa na kuzoea mazingira ya ushindani makubwa," alisema Oscar.
Serengeti Boys imepangwa Kundi A, pamoja na timu za Nigeria, Angola na Uganda huku B, likiwa na Guinea, Cameroon, Morocco na Senegar
Kikosi hicho, kimerudi na kinaendelea na kambi yao jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mashindano hayo.