Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Minziro apangua watatu, Ntibazonkiza abebeshwa mabomu

Kocha wa Geita Gold, Felix Minziro amedhamiria leo kuisimamisha Yanga ambapo amefanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kupangua wachezaji watatu huku akimrejesha beki wa kushoto, Adeyum Salehe ambaye hajaanza tangu alipocheza dhidi ya Azam na kufunga bao kwa mkwaju wa faulo.

Katika mabadiliko hayo matatu, Minziro amewapumzisha winga, Offen Chikola aliyefunga bao kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Deusdedith Okoyo na beki wa kushoto Yahya Mbegu ambaye amekuwa akianza katika mechi nyingi za timu hiyo.

Geita Gold ni wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Nyota watatu walioaminiwa leo ambao hawakuanza katika mchezo uliopita ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Ruvu Shooting ni beki Adeyum Salehe, kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma na winga, Raymond Masota.

Kikosi cha Geita Gold kinachoanza leo ni Arakaza McArthur, George Wawa, Adeyum Salehe, Oscar Masai, Kelvin Yondani, Yusuph Kagoma, Raymond Masota, Jofrey Manyac, Daniel Lyanga, Saido Ntibazonkiza na Juma Mahadhi.

Kikosi cha akiba ni Sebusebu Samson, Yahya Mbegu, Shawn Oduro, Bakari Hussein, Amosi Kadikilo, Deusdedith Okoyo, Ramadhan Chombo, Miraji Athuman na Offen Chikola.