Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda afichua kilichomtoa AS Vita

MGUNDA Pict

Muktasari:

  • Mgunda wakati yupo Mashujaa alifunga mabao mawili na asisti nne, aliliambia Mwanaspoti juu ya safari nzima ilivyokuwa hadi kutemana na AS Vita ndani ya muda mfupi kwani kwa sasa yupo nje ya kazi akisubiri msimu uishe aanze maisha mengine kwa ajili ya msimu ujao.

BAADA  kimya cha muda mrefu cha mshambuliaji Ismail Mgunda, hatimaye ameelezea sababu ya kuachana na AS Vita ya DR Congo aliyokuwa imemsajili akitokea Mashujaa inayocheza Ligi Kuu Bara.

Mgunda wakati yupo Mashujaa alifunga mabao mawili na asisti nne, aliliambia Mwanaspoti juu ya safari nzima ilivyokuwa hadi kutemana na AS Vita ndani ya muda mfupi kwani kwa sasa yupo nje ya kazi akisubiri msimu uishe aanze maisha mengine kwa ajili ya msimu ujao.

“Niliachana na AS Vita sikulipwa miezi mitatu, jambo lililofanya nishindwe kumudu maisha ya Kongo ambako mchezaji anajitegemea kila kitu chakula, sehemu ya kulala, tofauti na Tanzania kuna kambi na chakula kinakuwa juu ya timu,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Sikuwa na namna nyingine zaidi ya  kuwafuata viongozi na kuwaambia itakuwa ngumu kwangu kuendelea kuitumikia timu, tukafikia makubaliano yaliyoacha amani kwa pande zote mbili.”

Alisema makubaliano yalikuwa ni AS Vita isimlipe pesa za mkataba uliyokuwa umesalia bali impe barua ya kumuacha huru, ili akipata timu nyingine iwe rahisi kusajiliwa.

“Kwa sasa nipo nyumbani nafanya biashara zangu za vifaa vya umeme, ila kuna wakati nakumbuka kucheza, maana ndiyo kazi yangu,” alisema nyota huyo wa zamani wa Ruvu Shooting, Jomo Cosmos ya Afrika Kusini na Ihefu (sasa Singida Black Stars), aliyekuwa na ndoto kwa msimu huu kufunga mabao 10 katika Ligi Kuu kabla ya kutimkia DR Congo akiwa na amefunga mawili.