Adebayor: Tulistahili fainali FA

Muktasari:
- Singida ilianza kuvaana na Simba kwenye Uwanja wa KMC Complex, ikiwa ni kiporo cha Ligi Kuu Bara iliyopigwa Mei 28 jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, Wekundu wakishinda bao 1-0 kabla ya kwenda kukutana tena katika nusu fainali ya Shirikisho mjini Babati.
MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars, Victorien Adebayor amesema mechi mbili walizocheza dhidi ya Simba, waliwazidi wapinzani kiuwezo licha ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 1-0 na kwamba fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) iliwastahili kwa namna walivyofunika Manyara.
Singida ilianza kuvaana na Simba kwenye Uwanja wa KMC Complex, ikiwa ni kiporo cha Ligi Kuu Bara iliyopigwa Mei 28 jijini Dar es Salaam ikiwa kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, Wekundu wakishinda bao 1-0 kabla ya kwenda kukutana tena katika nusu fainali ya Shirikisho mjini Babati.
Katika mchezo huo wa Shirikisho, Simba ilipasuka kwa mabao 3-1 na kuifanya ipoteze taji la pili mfululizo kwa msimu huu ndani ya wiki moja baada ya awali kulikosa Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia mechi zote hizo ambazo alicheza, Adebayor aliliambia Mwanaspoti kwamba Singida ilipaswa kushinda mechi zote mbili.
“Kuanzia mechi tuliyofungwa bao 1-0 tulicheza kwa kiwango cha juu, wakati mwingine huwezi kujaji sana kinachotokea uwanjani, lakini kile tulichokifanya mechi ya FA kimedhihirisha uwezo wetu,” alisema nyota huyo raia wa Niger aliyeongeza; “Sina maana Simba haina kiwango kizuri, nazungumzia mechi mbili tulizokutana nayo siku za hivi karibuni, jambo la kufurahisha zaidi tumefuzu fainali.”