Mganda Biashara United apewa zigo kwa Yanga

Tabora. Baada ya kukosekana uwanjani kwa takribani mwezi mmoja huku akizikosa mechi tatu, Kipa wa Biashara United, James Ssetuba leo amepewa jukumu la kuhakikisha analinda lango.
Ssetuba alikosa michezo mitatu ya Ligi Kuu akimpisha Kipa namba moja wa timu hiyo, Daniel Mgore ikiwa ni dhidi ya Azam, Namungo, JKT Tanzania.

Mganda huyo ambaye ni msimu wake wa kwanza kukipiga hapa nchini ndiye amepewa nafasi ya kuanza leo golini chini ya Kocha raia wa Kenya, Patrick Okumu akimpumzisha mpinzani wake Mgore.
Kikosi cha Biashara United hiki;
James Ssetuba
Boniface Maganga
Mpapi Nassib
Leny Kisu
Abdulmajid Mangalo
Ibrahim Ndunguli
Ally Kombo
Ramadhan Chombo
Yusuph Athuman
Benson Masige
Deogratias Judike
Benchi wapo;
Daniel Mgore, Derick Mussa, Baraka Makoba
Tariq Simba,Christian Zigah, Kelvin Friday na Denis Nkane.