Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi wa Prisons awaacha hoi mashabiki Kyela, Prisons ikitinga fainali

Muktasari:

  • Roland bado hajasajiliwa ambapo anapambania namba na leo alikuwa  kivutio kutokana na kiwango alichoonesha hadi kuwakuna benchi la ufundi na mashabiki waliokuwa uwanjani hapo

Kyela. Wakati Prisons ikiifuata Baka City hatua ya fainali baada ya kuichakaza Mbeya Kwanza mabao 3-2 kivutio kilikuwa kwa straika wake Messi Roland ambaye aliwapagawisha mashabiki kwa kimo na kiwango alichoonesha uwanjani.

Nyota huyo ambaye alipita African Sports ya jijini Tanga ya Championship msimu uliopita,  kwa sasa yupo kwa Wajelajela hao akijaribu bahati kusaka namba kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao.

Straika huyo mrefu aliwavutia wengi kwani licha ya kuwazidi urefu wachezaji wote uwanjani, lakini hata vyenga vyake viliwakuna wengi na kumfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Fredi Felix  'Minziro' kubaki akicheka.

Staa huyo raia wa Afrika Kusini hakuishia kupiga vyenga bali ndiye alianza kuwatanguliza Prisons kwa bao la kwanza kabla ya Edwine Balua kuongeza la pili na tatu kufikisha matano hadi sasa na kuongoza kwenye orodha ya wafungaji.

Ikumbukwe kuwa hadi sasa Maafande hao katika usajili wao wametamburisha mchezaji mmoja, Salum Kihimbwa, huku nyota wengine akiwamo Eliud Ambokile,  Hamis Kassanga, Chilo Mkama na Messi wakiwa kwenye uangalizi.

Katika mchezo huo Prisons walionekana kuwazidi Mbeya Kwanza kwa kuutawala zaidi mpira na kuweza kutangulia mabao mawili ya mapema yaliyodumu hadi mapumziko.

Mbeya Kwanza wanaojiandaa na championship msimu ujao hawakuondoka patupu walipopata bao la kwanza dakika ya 69 kupitia kwa Frank Athanas kabla ya  Oscar Mwajanga kutupia la pili kwa penalti dakika ya 88.

Kuingia kwa bao hilo lililnekana kuwachanganya Prisons, ambapo benchi la ufundi lilionesha kutokubaliana na uamuzi wa refa lakini Balua aliweza kupiga mpira wa faulo ulioenda hadi wavuni na kuihakikishia timu hiyo kufuzu fainali.

Kwa matokeo hayo Prisons watakipiga kesho Jumatano dhidi ya Baka City ya Malawi kwenye fainali ya Samia MbeyaPreSeason, huku Mbeya Kwanza na Mbeya City wakiumana kusaka mshindi wa tatu mechi zote zikipigwa kesho Jumatano.