Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya Kwanza, KMC hakuna mbabe

Mbeya. Bao la dakika 90 lililofungwa na Straika Habibu Kyombo limeinusuru Mbeya Kwanza kuambulia pointi moja baada ya sare ya bao 1-1 waliyopata leo dhidi ya KMC.

Kabla ya mchezo huo, Mbeya Kwanza walikuwa wakikumbuka kisago cha bao 1-0 dhidi ya Azam, huku KMC wakitakata mbele ya Tanzania Prisons kwa mabao 2-0.

Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini hapa, timu zote zilionrkana kukamia haswa wenyeji Mbeya Kwanza waliotumia nguvu kulazimisha mashambulizi lakini hadi dakika 45 za awali zinamalizika, hakuna aliyeona lango la mwenzake.

Straika wa Mbeya Kwanza, Habibu Kyombo manusura aihakikishie bao timu yake baada ya mpira wake uliojaa wavuni dakika ya 17 mwamuzi wa pembeni, Frank Chavala kuashiria ameotea na refa, Amina Kyando (Morogoro) kukataa bao hilo.

Hata hivyo mchezaji Matheo Anthony alioneshwa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Mbeya Kwanza, Brown Mwankemwa dakika ya 28.

Kipindi cha pili kilianza timu zote zilishambuliana ambapo dakika ya 53, Anthony aliipatia bao KMC baada ya kutokea piga nikupigie na mfungaji huyo kuukwamisha mpira wavuni na kumuacha Kipa Hamadi Kadedi akikosa la kufanya.

Mbeya Kwanza walipambana kusawazisha bao hilo, lakini Kipa Farouk Shikhalo alionekana kuwa imara kudaka mashuti yote yaliyolenga lango lake, huku mabeki wake nao walifanya kazi nzuri.

Dakika ya 73 na 86, KMC iliwapumzisha Hassan Kabunda, Matheo Anthony, Ismail Gambo na Emanuel Mvuyekile na nafasi zao kujazwa na Saddath Mohamed, Miraji Athuman Mohamed Kipagwile na Abdalah Masoud huku Mbeya Kwanza wakimtoa Oscar Mwajanga na kumwingiza Hamis Kanduru dakika ya 80.

Mabadiliko hayo yaliwanufaisha Mbeya Kwanza kwa kusawazisha bao dakika ya 90 kupitia kwa Kyombo aliyesukuma mpira kwa kisigino kufuatia faulo iliyopigwa na Miza Christom na kuwafanya KMC kuondoka na alama nne ugenini baada ya mechi iliyopita kuwaua Prisons mabao 2-0.