Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe amlia kiapo Emmanuel Amunike Star

Muktasari:

Akizungumzia kilichoiponza Serengeti Boys hadi kuondolewa kwenye mashindano ya AFCON hatua ya makundi, alisema walizidiwa kila nyanja.

BERTHA ISMAIL, ARUSHA

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ Kelvin John ‘Mbappe’ ameshukuru kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake, Emmanuel Amunike na kuahidi kuitendea haki nafasi hiyo.

Mbappe amekuwa miongoni mwa nyota 39 walioitwa kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu, nchini Misri.

“Nashukuru kupata nafasi hii na kwa msaada wa Mungu nitafanya yale yote ambayo ataniagiza yeye nifanye chini ya maelekezo yake na naamini nitaweza kupambana kwa sababu nina maarifa na uwezo pia ninao, nitafanya kwa vitendo maagizo nitakayopewa na mwalimu kuisadia timu ipate matokeo.”

Kelvin aliwaondoa hofu wadau wa michezo nchini wanaomhukumu kwa umri wake mdogo na kusema kuwa kipaji hakiangilii umri kwani uwezo mkubwa alionao ni wa kupambana hivyo kuwaomba dua Watanzania katika safari yake ya kuisaidia Taifa Stars kupata matokeo.

Kelvin pia aliwapa somo wachezaji wenzake walioitwa kwenye kikosi hicho kuhusu timu walizopangwa nazo kundi moja la Afcon kwamba ni lazima wakawakabili kwa tahadhari.

Akizungumzia kilichoiponza Serengeti Boys hadi kuondolewa kwenye mashindano ya AFCON hatua ya makundi, alisema walizidiwa kila nyanja.

“Tulizidiwa uwezo, mipango na mbinu ndio maana tulifanya vibaya na kila mtu anajua tulifanya vibaya. Naomba radhi kwa Watanzania kwa hilo kwani halikuwa matarajio yetu na yaliyotokea hata sisi tuliumia,” alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 16.