Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele: Kufunga ni akili, mabeki ni wagumu

PAMOJA na Azam FC kutunguliwa mabao 2-0 na Yanga, straika Fiston Mayele amesema alikutana na ugumu wa mabeki, lakini kilichomsaidia ni akili muda wote akaweza kucheka na nyavu.

Mayele aliliambia Mwanaspoti kwamba, mabeki wa Azam FC siyo wabaya isipokuwa soka ni mchezo wa makosa waliyoyatumia kuwaadhibu na kupeleka kicheko Jangwani.

Staa huyo anamiliki mabao matatu - moja alifunga mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Simba, mawili ya Ligi Kuu akisema hakuna mechi rahisi kinachotakiwa ni upambanaji na umakini wa kutumia nafasi.

“Tumewafunga Azam FC haina maana kwamba beki yao ilikuwa mbovu. Walifanya makosa na umakini wetu ukafanya tuwaadhibu, hilo ndilo naweza nikalisema katika mchezo huo,” alisema.

Kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ licha ya kutokuwa na timu kwa sasa, anahudhuria viwanjani kuangalia kinachotokea, ndiyo maana ilikuwa rahisi kumzungumzia Mayele.

“Mayele ni straika ambaye akili yake imekaa golini, maana bila kufunga siyo rahisi timu kupata mafanikio. Anajua kuzitumia nafasi kama alivyokuwa anafanya Meddie Kagere misimu miwili iliyopita ambayo kipa ukimuona lazima akili itulie muda wote,” alisema.

Kipa chipukizi wa Mtibwa Sugar, Aboutwalib Mshery alisema Mayele ni kati ya mastraika anaowatazama ili wakikutana asiwe na madhara kwenye lango lake.