Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maureen Sizya apika watu Sauzi

SIZYA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanasposti baada kurejea nchini juzi, Maureen alisema BAL4HER ni mpango unaolenga kuibua, kuendeleza na kuwawezesha wanawake wa Kiafrika katika nyanja ya uongozi wa michezo, huku pia wakifundisha.

MTANZANIA Maureen Sizya ni mmoja wa makocha wa kikapu katika jopo la mradi ya BAL4HER nchini Afrika Kusini, alikoungana na wakufunzi mahiri kutoka Amerika, Afrika Kusini na Gabon kufundisha umahiri wa mchezo huo.

Akizungumza na Mwanasposti baada kurejea nchini juzi, Maureen alisema BAL4HER ni mpango unaolenga kuibua, kuendeleza na kuwawezesha wanawake wa Kiafrika katika nyanja ya uongozi wa michezo, huku pia wakifundisha.

“Kupitia mpango huu makocha wanawake huchaguliwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika ili kupata mafunzo, uzoefu wa kitaalamu na fursa za kushirikiana na wakufunzi wa kiwango cha kimataifa,” alisema.

Alisema wakiwa nchini Afrika Kusini walipata nafasi ya kufundisha nyota wa umri wa miaka 23 wakati wa fainali ya  mashindano ya ubingwa wa Afrika maarufu kama BAL.

Mbali ya kuwa kocha, pia ni mchezaji wa timu ya Tausi Royals inayoshiriki Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam upande wa wanawake (WBDL).