Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki watumia njia mbadala kupenya uwnajani kuwaona Simba

Vijana wakitumia mbinu yao kupenya kuingia uwanjani kupitia kwenye mageti yaliyofungwa ili kushuhudia mchezo wa Mwadui na Simba.Picha na Saddam Sadick

Muktasari:

Hadi sasa bado milango haijafunguliwa huku ikielezwa kuwa mashabiki wataanza kuingia uwanjani kuanzia saa 6:30 mchana ambapo kiingilio ni Sh 5000 mzunguko na Sh 10,000 jukwaa kuu.

Shinyanga. Ikiwa hata bado mashabiki kuruhusiwa kuingia uwanjani, tayari baadhi wameanza kuingia wakitumia njia za mkato.

Mwanaspoti Online ambayo iko viunga hivyo vya uwanja wa CCM Kambarage, imeshuhudia vijana mbalimbali wakiingia uwanjani wakitumia nyufa kwenye mageti yaliyozunguka dimba hilo.

Vijana hao ambao hawakufahamika haraka majina yao, walikuwa wamejipanga foleni kila mmoja akisubiri mwenzake apenye kisha mwingine kufuata.

Mashabiki Simba waihofia Mwadui Fc || Chama, Miquissone kubeba matumaini yao 'Mwadui nayo ni timu'

Mchezo wa Mwadui na Simba unatarajia kupigwa leo saa 10 jioni ambapo imeelezwa kuwa milango itaanza kufunguliwa saa 6:30 mchana kutokana na idadi kubwa ya mashabiki.

Bila kujali usalama wao, vijana hao walionekana kufurahi mbinu hiyo wakidhani wamewaweza walinzi wa getini aidha kwa kukosa kiingilio au kunusuru pesa zao.

Hata hivyo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Jamal Ahamad ambaye alikuwa makini kufuatilia tukio zima, amesema hajaelewa ujanja wanaoutumia vijana hao kwani eneo ni dogo lakini wanapenya kirahisi.

"Unajua nimeshangaa kwa sababu eneo ni dogo sana lakini wanapenya kirahisi, ila katika hali nyingine wanaweza kupata tatizo kubwa" amesema Ahmad.