Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Masanja,Mbasha kukiwasha kwenye Injili

Muktasari:

Baadhi ya watangazaji wanaounda timu yao kuwa ni Boniface Magupa, Victor Aaron, Douglas Pius DP, Ben Bonge, Silas Mbise, Alphonce Mutema, Jonh Kisaka na Hosein Gabriel.

USIDHANI wanaimba nyimbo za Injili tu, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ na Emmanuel Mbasha watakipiga katika mpambano wa kirafiki unaohusisha waimbaji na watangazaji mbalimbali.

Msemaji wa mchuano huo, Hosein Gabriel alisema mchezo huo wa kirafiki utafanyika kwenye Uwanja wa Kenton High School, Mwenge jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii kuanzia saa 1.00 asubuhi.

Gabriel alisema mbali na mastaa hao, wengine wanaounda kikosi cha Muziki wa Injili ni Stanley Msungu, Anania Mwasomola, Peter Banzi, Daniel Thomas, Gazuko Junior

“Tunataka kujenga urafiki baina yetu kwa sababu wote tunafanya kazi moja kupeleka ujumbe wa Mungu kwa jamii kwa hiyo, niwaombe mashabiki wetu waje watazame mchuano huu kabambe,” alisema.

Aliwataja baadhi ya watangazaji wanaounda timu yao kuwa ni Boniface Magupa, Victor Aaron, Douglas Pius DP, Ben Bonge, Silas Mbise, Alphonce Mutema, Jonh Kisaka na Hosein Gabriel.