Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MARA PAAP!!! SITAKI KUWEKWA KWENYE ORODHA YA WANAUME

Mwigizaji huyo ambaye majina yake kamili ni Blandina Chagula

Muktasari:

Mwigizaji huyo ambaye majina yake kamili ni Blandina Chagula, ni miongoni mwa waasisi wa Bongo Movie ya kileo, baada ya kundi la wasanii wa Kaole kujitosa kwenye uigizaji wa filamu na kufunika kinomanoma hadi leo.

NI vigumu kutaja mafanikio wa sanaa ya uigizaji nchini bila kiulitaja jina la Johari, mwanadada aliyetambulishwa kwenye sanaa hiyo kupitia Kundi la Kaole Sanaa.

Mwigizaji huyo ambaye majina yake kamili ni Blandina Chagula, ni miongoni mwa waasisi wa Bongo Movie ya kileo, baada ya kundi la wasanii wa Kaole kujitosa kwenye uigizaji wa filamu na kufunika kinomanoma hadi leo.

Sura ya Johari, akiwa sambamba na marehemu Steven Kanumba enzi zake za uhai, Vincent Kigosi ‘Ray’, Chiki Mchoma, Makhsein Awadhi ‘Dk Cheni’ na wengine zilipamba kava za filamu nyingi na kupapatikiwa kutokana na umairi wao.

Kwa sasa Johari ni kama umri unamtupa mkono, lakini bado mwanadada huyo anaendelea kukamua akiwa ni mtayarishaji wa filamu mbali na uigizaji na Mwanaspoti limemnasa na kupiga naye stori mbili tatu. Kubwa ni kusisitiza asivyopenda kupakaziwa mambo ya uzushi na kudhalilishana. Kivipi? Tiririka naye..!

Mwanaspoti: Habari yako Johari?

Johari: Nzuri tu, habari yako nawe?

Mwanaspoti: Nzuri kabisa, vipi Johari umepoa sana dada’ake, kiasi cha kuwafanya wasanii kibao wameibuka na kulifunika jina lako, kulikoni?

Johari: Unajua siku zote avumae baharini ni papa kumbe wengine wapo, hivyo hainipi shida kuibuka kwa wasanii wapya au wanaoibuka kwani natambua vizuri jinsi ninavyofanya kazi.

“Kwa maana mimi ni mtunzi na muongozaji, hivyo mara nyingi nakaa nyuma ya kamera, hivyo ni rahisi kutotamba kama zamani nikiigiza.

Mwanaspoti: Mbona hukuhudhuria Tamasha la ZIFF 2018? Na kwanini wasanii wenye majina wengi wenu mliingia mtini safari hii?

Johari: Binafsi sikushiriki kwa vile nilikuwa Mwanza kwenye kazi niliyoingia mkataba kwa siku hizo, ila suala la kutoshiriki kwa wingi, hilo sijafahamu kwa wenzangu ila mimi majukumu yalinibana na ninatambua umuhimu na faida ya tamasha hilo.

Mwanaspoti: Tutegemee lini ndoa yako? Maana umri unaenda mama!

Johari: Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, hivyo nina kiu ya kuwa na mume. Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuolewa kwa ajili ya fasheni ama kukurupuka kwa vile tu msanii fulani ameolewa. Ndoa ni mipango.

Mwanaspoti: Mtu akikwambia umpe kwa ufupi historia yako ya mapenzi utamwambiaje?

Johari: Mapenzi yamenifundisha mengi, najielewa na kujitambua vizuri. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Johari wa zamani na wa sasa. Kwanza nimekomaa kiakili, nimekutana na vitu vingi na nimejua maisha ni nini. Nipo tayari kufanya maisha na mwanaume aliye siriazi.

Mwanaspoti: Mastaa wengi wamekuwa wakiweka wazi uhusiano wao wa kimapenzi wazi, mbona wewe umekuwa ukiyaficha kwanini?

Johari: Sio kama nayaficha, bali niliyenaye bado sijafikia kumnadi kwa watu, naepuka kumuonyesha mtu leo kesho mnamwagana halafu nami nikaingizwa kwenye orodha ya mwanaume huyo au kutajwa kati ya wenye listi ya wanaume wengi.

Mwanaspoti: Kuna habari zinadai kuwa, sikuhizi umekuwa mtu wa kilevi hadi unapitiliza, hii ni kweli?

Johari: We mwenyewe unanijua Rhobi, sidhani kama kuna ukweli kuhusu hilo, lakini hata ikiwa hivyo, hakuna mtu anayemzuia mtu kufanya kitu anachopenda.

Mwanaspoti: Una ushauri gani kwa wasanii wenzako?

Johari: Nawashauri tupendane na tuache kushabikia mambo mabaya yawapatayo wengine, badala yake tuungane kwa pamoja ili kusaidiana kwani sisi ni wamoja.

Kwenye misiba hali ni nzuri tupo pamoja, lakini kwenye majanga mengine tunatupana, hatutakiwi kuchekana, badala yake tupeane moyo na ushauri wa jinsi ya kutoka huko.

Mwanaspoti: Kitu gani hukipendi?

Johari: Kuandikwa vibaya katika media na hasa kwa uzushi wa mambo ya kudhalilishana, yaani vitu hivi vinakwanza na kukatisha tamaa katika uigizaji.

Mwanaspoti: Shukrani sana ndugu yangu.

Johari: Asante na karibu tena!