Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mamilioni yatuliza mzuka wote Yanga, watinga kambini

Muktasari:

Wachezaji wa Yanga walikuwa kwenye mgomo wa kutofanya mazoezi kwa siku mbili wakidai posho na malipo mbalimbali

Dar es Salaam. Hakuna tena mzozo ndani ya Yanga na hali ni shwari, lakini kazi iliyobaki kwa sasa ni moja tu na ahadi iliyotolewa ni kwamba, Azam FC anapigwa mapema.

Iko hivi. Wachezaji wa Yanga walikuwa kwenye mgomo wa kutofanya mazoezi kwa siku mbili wakidai posho na malipo mbalimbali, ambapo jitihada za uongozi na kocha zikachukua nafasi yake.

Kwanza ilionekana kuwa suala gumu kumalizwa mapema na kumlazimu Kocha Mwinyi Zahera, kuonya kuwa watakaoshindwa kufika mazoezi basi wamejiondoa kwenye kikosi chake.

Sasa si unajua Zahera huwa hana utani katika kusimamia maamuzi yake kama alivyofanya kwa kipa Beno Kakolanya, sasa mambo yamekwisha kwenye uwanja huo huo wa mazoezi pale Kurasini, baada ya matajiri wa Yanga kushusha mamilioni ya fedha na kumaliza kesi.

Juzi, kulikuwa na mzozo wa malipo wa wachezaji na uongozi wa timu hiyo ambao ulimalizwa kwa kikao kilichowahusisha wachezaji na kamati maalum ya kusimamia timu chini ya Mwenyekiti wake, Lucas Mashauri aliyeambatana na baadhi ya wajumbe wake.

Sasa jana uwanjani hapo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi, Mwanaspoti lilishuhudia wachezaji hao wakiondoka kwa roho safi baada ya vigogo hao kuweka mambo sawa na kuwalipa baadhi ya madai yao kama walivyokubaliana.

Wakiwa ndani ya uwanja huo wa mazoezi pale Chuo cha Polisi Kurasini, Mwanaspoti lilimshuhudia mratibu wa timu hiyo Hafidh Saleh akizungumza na wachezaji hao pamoja na manahodha kisha kugawana fedha.

Baada ya mgawanyo huo kila mchezaji alionekana akiwa na furaha, ambapo sasa akili yote ni mchezo dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Uwanja wa Uhuru.

"Tumewalipa fedha walizokuwa wanadai hasa posho baada ya kukaa na kutuelewesha wanataka kitu gani, kamati tukaona tulimalize hilo na wenyewe wameahidi watafanya kazi,” alisema mmoja wa vigogo wa kamati hiyo, ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Jeshi kambini

Katika kuonyesha kuwa mambo ni shwari, jana jioni kikosi kamili kiliingia kambini palepale kwenye hoteli ya Nefland iliyopo Manzese, Dar es Salaam tayari kwa kuiwinda Azam.

Kabwili kama Diamond

Kipa kinda wa timu hiyo Ramadhan Kabwili kama hataondoa basi ataibuka katika mchezo huo akiwa na sura mpya baada ya kuweka rasta kichwani huku wenzake wakimpa jina jipya.

Kabwili alionekana jana akiwa na rasta kichwani ikiwa ni mtindo mpya kwake tangu asajiliwe na timu hiyo na kuwafanya wenzake kumuita Diamond Platnumz, ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva.

Wakiwa mazoezini hapo kipa mwenzake Klause Kindoki na hata nahodha Ibrahim Ajib walisikika wakimuita jina la Diamond huku mwenyewe akichukulia poa tu.