Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo matatu kwa Biashara United vs Yanga

Muktasari:

Kabla ya mechi ya leo Ijumaa, timu hizo zimekutana mara saba ikiwa sita za Ligi Kuu na moja ya kombe la shirikisho ambapo Yanga imeshinda tano, sare moja na kupoteza moja.

Tabora.Wakati mashabiki na wadau wa soka wakisubiri kwa hamu mechi ya nusu fainali ya kwanza ya kombe la shirikisho kati ya Biashara United na Yanga, mchezo huo umeonekana kubebwa na rekodi, visasi na heshima ndani ya uwanja.

Timu hizo zinatarajia kushuka uwanjani leo Ijumaa saa 9:30 mchana katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa, huku kila upande ukihitaji ushindi ili kufuzu hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Katika mchezo wa leo licha ya timu zote kutamba kushinda, lakini imeonesha rekodi kuwabeba zaidi Yanga ambao katika michezo saba waliyokutana na wapinzani wao, wameishinda tano, sare moja na kupoteza moja.

Pamoja na Yanga kujivunia rekodi hiyo, lakini imekuwa ikipata upinzani mkali na kufanya mchezo wa leo Biashara United kuhitaji heshima kutokana na ubora waliouonesha katika mashindano yao ya Ligi Kuu na shirikisho.

Pia timu hiyo ya mjini Musoma itahitaji ushindi ili kufuta 'uteja' na kulipa kisasi dhidi ya wapinzani wao ili kutinga hatua ya fainali kwa mara ya kwanza.

Kwa upande wa Yanga watahitaji ushindi ili kuweka matumaini ya kutwaa ubingwa huo kutokana na hesabu za kwenye Ligi Kuu kuwa ngumu hivyo kufanya mechi ya leo kuwa na ushindani mkali.