Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malale awajia juu mastaa JKT

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Malale Hamsini amesema sababu kubwa ya timu hiyo kushindwa kutamba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ni kutokana na wachezaji wa kikosi hicho kupoteza umakini mwishoni.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 huku JKT ikitangulia kupitia kwa Daniel Lyanga kisha Gasper Mwaipasi kusawazisha mwishoni kabisa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Malale alisema walistahili kuondoka na pointi tatu katika mchezo huo ila kitendo cha kukosa umakini na nidhamu kubwa kwenye uzuiaji ndio sababu iliyowafanya kusawazishiwa kirahisi bao hilo.

"Baada ya kupata bao dakika zile za jioni wachezaji waliamini tayari mchezo umeisha hivyo kupoteza umakini kwenye uzuiaji na kuruhusu wapinzani wetu kusawazisha, tunarudi uwanja wa mazoezi kulifanyia kazi," alisema.

Malale aliongeza licha ya kutowapa furaha mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuwapatia sapoti ila amewataka waendelee kuisapoti timu hiyo kwani makosa waliyofanya watayarekebisha kabla ya kucheza na Mashujaa, Oktoba 3.

Mchezo huo ni wa nne kwenye Ligi Kuu Bara kwa JKT msimu huu ambapo ilianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo kisha ikachapwa mechi mbili mfululizo ikianza na kichapo cha mabao 5-0 kutoka kwa Yanga, 2-1 na KMC.