Makata aitumia Ruvu kuifunga Simba

Muktasari:
Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata, ameingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba akianza na kikosi kilichoifunga Ruvu Shooting.
Dodoma. Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata, ameingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Simba akianza na kikosi kilichoifunga Ruvu Shooting.
Katika mchezo huo uliochezwa Jumanne wiki hii uwanja wa Jamhuri, Makata alianza na kikosi kile kile kilichofanikiwa kufunga bao kipindi cha kwanza lililodumu hadi mwisho wa mchezo.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 33 na kiungo wa kati, Cleophas Mkandala, likadumu hadi filimbi ya mwisho wa mchezo huo uliokua mgumu kwa timu hizo.
Kipa chaguo la tatu msimu uliopita, Hussein Dotto (mtoto wa nyumbani) ameendelea kuaminiwa mbele ya makipa Mohammed Yusuph aliyekua kipa namba moja wa Polisi Tanzania pamoja na Rahim Sheikh aliyetokea KMC.
Upande wa beki wa kulia anacheza George Wawa, kushoto ni Abubakar Ngalema, mabeki wa kati ni Nahodha Mbwana Kibacha na Augustino Nsata.
Viungo ni Salmin Hoza na Cleophas Mkandala wakati mawinga wa kulia na kushoto ni David Ulomi na Jamal Mtegeta.
Washamhuliaji wa kati ni Anuary Jabir na Mcha Khamis ambao wameanza mbele ya Seif Karihe na Omary Kanyoro.