Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa: Yanga tayari, bado wenye nchi

Muktasari:

  • Jana klabu ya Yanga ilihitimisha kilele cha Wiki ya Mwananchi na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya  Kaizer Chief ya Afrika Kusini katika uwanja wa Benjamini Mkapa  ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Kennedy Musonda

Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki mbio za NBC Marathoni huku akisema kilele cha wiki ya Wananchi  kimepita  inayosubiriwa ni  siku ya wenye Nchi.

Jumamosi ,Julai 22,2023 klabu ya Yanga ilihitimisha kilele cha wiki ya mwananchi kwa kucheza na Kaizer Chief ya Afrika Kusini katika uwanja wa Benjamini Mkapa  ambapo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Kennedy Musonda.

Akizungumza   leo Jumapili Julai 23 katika mbio za NBC Marathoni katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa Majaliwa amesema baada ya mchezo wa jana sasa kinachosubiriwa ni siku ya Simba Day Agosti 6 mwaka huu.

“Niwakumbushe jana ilikuwa siku ya wananchi,  Yanga  inajiandaa kuingia katika ligi kuu,sasa  tarehe 6 ni siku ya wenye nchi,nao wanajindaa, kuna wenye nchi na wananchi lakini kuna Azam, Namungo na Singida Big Stars hii yote ni hamasa iliyotolewa  na NBC,”amesema Majaliwa

Waziri Mkuu ameipongeza benki ya NBC kwa kuandaa mbio huku akizitaka taasisi zingine kuiga mfano huo.
Amesema Serikali inahitaji kuona kila taasisi ikipambana kuhakikisha sekta ya afya inazidi kuboreka nchini.

“Nitumie nafasi hii kuipongeza NBC kwa kuendeleza michezo piga makofi kwa NBC, watanzania mnajua benki hii ndio wadhamini wakuu  wa ligi kuu ambayo ni ligi maarufu na inachukua nafasi ya tano, hizi ni jitihada za NBC,”amesema Waziri Mkuu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema kupitia mbio hizo jumla ya Sh300 milioni zimepatikana na zitaenda moja kwa moja kwenye matibabu ya  kansa ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kwenye taaluma ya ukunga nchini.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoPindi Chanaamesema  wamedhamiria kuwaondoa wagonjwa kwenye vitanda kwa kutumia mfumo wa ufanyaji mazoezi kuanzia ngazi ya mtaa.