Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bwenzi aitosa Coastal atimkia Mashujaa

BWENZI Pict

Muktasari:

  • Mashujaa iliyo na mechi mbili kabla ya kufunga msimu wa 2024-2025, imeanza kusaka nyota wapya kwa ajili ya kujipanga kwa msimu ujao, na inaelezwa imeshamalizana na Bwenzi baada ya kuamua kuzitosa timu zilizokuwa zikimnyatia tangu ifahamike KenGold imeshuka daraja.

MAAFANDE wa Mashujaa wameshinda vita ya kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa KenGold,  Selemani Rashid ‘Bwenzi’ aliyekuwa akiwindwa na Coastal Union, JKT Tanzania na Tabora United.

Mashujaa iliyo na mechi mbili kabla ya kufunga msimu wa 2024-2025, imeanza kusaka nyota wapya kwa ajili ya kujipanga kwa msimu ujao, na inaelezwa imeshamalizana na Bwenzi baada ya kuamua kuzitosa timu zilizokuwa zikimnyatia tangu ifahamike KenGold imeshuka daraja.

Mwanaspoti lilikuwa linafahamu kiungo huyo alikuwa karibu kumalizana na Coastal, lakini walishindwana upande wa dau la kusaini mkataba.

Taarifa za ndani zimeliambia Mwanaspoti kuwa, “jamaa ametimkia Mashujaa kweli na tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili.”

Chanzo cha habari kutoka mtu wa karibu wa mchezaji kiliongeza: “Mashujaa imempa mkataba wa miaka miwili japokuwa siwezi kuweka wazi kiasi cha pesa ila msimu ujao atakuwa na jezi mpya.”

Bwenzi  alianza kuitumikia KenGold kuanzia dirisha dogo lililofungwa Januari akiwa ameifungia mabao matano na kung’ara miongoni mwa nyota wa timu hiyo, licha ya kikosi hicho kutokuwa na msimu mzuri kwani imeicheza msimu mmoja kabla ya kushuka sambamba na Kagera Sugar.

Mashujaa ipo katika nafasi ya nane ikiwa imecheza mechi 28 ikiwa na pointi 33, ikishinda nane, sare tisa na kupoteza 11 ikifunga mabao 28 na kufungwa 32, na ikiwa katika hatari ya kuangukia katika mechi za mtoano kutoshuka daraja.

Timu hiyo ya mjini Kigoma itamaliza msimu ikiwa nyumbani ikiwa imesalia na mechi mbili dhidi ya KMC na JKT Tanzania kabla ya kuanza mipango kwa ajili ya msimu ujao ikiwa ni msimu wa tatu tangu ilipopanda daraja msimu uliopita ilipomaliza katika nafasi ya nane.