Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Luis anakuja mdogomdogo Simba

Muktasari:

  • Luis alitumika kwa dakika 90 na kocha alisema anamuona yule fundi anayesubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu hiyo kwani ameanza kurudi kwenye ubora wake.

SIMBA juzi ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam na kuipumulia Yanga kileleni zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa, lakini kuanza kuimarika kwa Luis Miquissone kumemfurahisha kocha, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Luis alitumika kwa dakika 90 na kocha alisema anamuona yule fundi anayesubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu hiyo kwani ameanza kurudi kwenye ubora wake.

Katika mchezo huo wa juzi, Luis alisababisha bao la tatu lililofungwa kwa penalti baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya boksi lakini alifanya kitendo kilichowakosha mashabiki kwa kumpa Baleke aliyekuwa amefunga mabao mawili akamilishe hat-trick’ yake, na kujinyima fursa ya kuandika bao lake la kwanza la msimu huu.

Kocha Robertinho alisema amefurahi kumuona nyota huyo akicheza kwa dakika zote 90 bila kuchoka.

“Awali alikuwa hawezi kufanya hivi, lakini tumemuona akizidi kuwa bora na kutochoka, hili ndilo tunalotaka kwani tukiwa wote kwenye ubora inatusaidia,” alisema Robertinho ambaye alikuwa anasema mara kwa mara mchezaji huyo hakuwa fiti kwa sababu alichelewa kujiunga na wenzake katika pre-season.

Robertinho alisema anafurahi kuona wachezaji wake wakizidi kuimarika kadri siku zinavyokwenda mbele na kwamba timu inakua kwa pamoja, jambo ambalo anajivunia kwani litamsaidia katika siku zijazo.

“Timu yangu ina makundi mawili, lakini yote yapo sawa kwa kulingana kwa sasa jambo ambalo linanipa nguvu katika kila mchezo unaokuja. Viwango vya wachezaji vinazidi kuimarika, hii inafurahisha.”

Kuhusu mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ya Zambia waliotoka nao 2-2, alisema wanajiandaa vyema.