Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lipumba hajakatwa, amejikata!

Prof. Ibrahim Lipumba

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa  Ibrahim Lipumba, yeye ameamua kujikata mwenyewe ndani ya chama hicho.

EDWARD Lowassa Waziri Mkuu wa zamani alikatwa CCM kwenye mbio za kuwania urais wa Tanzania kupitia chama hicho tawala, baadaye akahamia Chadema na kuteuliwa kuwania uras kupitia Ukawa.

January Makamba naye alikatwa, japo hakuhama CCM. Dk Makongoro Mahanga alikatwa kwenye ubunge na kuamua kuhamia Chadema.

Lakini  Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa  Ibrahim Lipumba, yeye ameamua kujikata mwenyewe ndani ya chama hicho.

Msomi huyo wa fani ya Uchumi, alitangaza uamuzi wake jana Alhamisi akiachia cheo chake za Uenyekiti ikiwa ni siku moja baada ya kuwapo minong’ono ya kujiuzulu kwake ambayo juzi Jumatano ilikanushwa na baadhi ya viongozi wa CUF.

Profesa Lipumba alisema amejiuzulu uenyekiti wa CUF lakini anaendelea kuwa mwanachana wa  kawaida baada ya kutokubaliana na baadhi ya mambo yanayoendeshwa ndani Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ni pigo jingine Ukawa unaoundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD  kwani awali Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa, aliamua kupumzika baada ya kutofautina na Kamati Kuu ya chama chake wakati wa kumpokea Lowassa.

“Leo hii nimeikabidhi ofisi ya Katibu Mkuu barua yangu ya kung’atuka nafasi ya Mwenyekiti wa taifa, lakini naendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yangu imelipiwa mpaka mwaka 2020,” alisema Profesa Lipumba.

“Nawaomba radhi sana wanachama na wananchi walioniamini na kuonesha mapenzi makubwa kwangu na katika uongozi wangu,” alisema.

“Nilishiriki katika mchakato wa kumkaribisha Lowassa, lakini baada ya kutafakari dhamira, ikanisuta.”