Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya Zanzibar yapata kocha Mzungu

Memik Vurucu (kushoto) kocha mpya wa Jang'ombe Boys baada ya kutua visiwani Zanzibar.

Muktasari:

Vuruc alitua juzi Jumamosi na ataanza kukifundisha kikosi hicho leo Jumatatu. Hii ni mara ya kwanza kwa Jang’ombe Boys kucheza Ligi Kuu Zanzabar na kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

IMEZOELEKA kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara kuajiri makocha wa kigeni hasa wazungu, lakini sasa hali hiyo imevuka maji mpaka huku Zanzibar kwani tayari timu ya Jang’ombe Boys imemuajiri kocha Mzungu kutoka Uturuki, Memik Vurucu.

Vuruc alitua juzi Jumamosi na ataanza kukifundisha kikosi hicho leo Jumatatu. Hii ni mara ya kwanza kwa Jang’ombe Boys kucheza Ligi Kuu Zanzabar na kocha huyo amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Juzi Vuruc alikuwepo uwanja wa Amaan akiwashuhudia mabingwa wa Ligi Kuu Zanzibar, Mafunzo, wakicheza na Mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam FC ambapo Mafunzo walifungwa mabao 3-0. Jang’ombe itakutana na Mafunzo kwenye mechi zao za ligi hiyo.

Katibu Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Dallas ameliambia Mwanaspoti kuwa kocha huyo atakuwa anasaidiana na mzawa, Issah Othuman ‘Amasha’.

“Kuna wadau wetu ambao ni wazawa wa hapa ila wanaishi Uturuki na mara nyingi wamekuwa wakitusaidia tulipokuwa ligi za chini, wameamua kutuletea kocha ambaye kila kitu watakuwa wanamlipa wao, tumesaini naye mkataba wa mwaka mmoja,” alisema.

“Hatutakuwa na kambi ya moja kwa moja ila watakuwa wakitokea nyumbani, tumebadilisha uwanja wa mazoezi kwani ule wa awali tuliokuwa tunautumia ni mbovu sasa tutatumia Uwanja wa Dimani nje kidogo ya mji.”

Kuhusu usajili alisema timu yao imesajili wachezaji kumi wapya lakini wote ni kutoka visiwani humu na mpaka sasa wameshafunga usajili wao kwa kuwa na wachezaji 30 ambao wanaamini wanao uwezo wa kufanya vizuri.