Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kyaruzi aitega Mtibwa Sugar

KYARUZI Pict

Muktasari:

  • Kyaruzi akiwa sehemu ya kikosi cha Mtibwa Sugar msimu huu katika Ligi ya Championship ameiwezesha kuwa bingwa na kupanda daraja kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka msimu uliopita. Mtibwa Sugar ilimaliza kileleni kwa pointi 71.

BEKI mkongwe wa zamani wa Kagera Sugar, Erick Kyaruzi ‘Mopa’ amesema ametimiza malengo aliyopewa na Mtibwa Sugar kuhakikisha anaisaidia kurejea Ligi Kuu Bara, huku akijivunia kutoa mchango mkubwa kwa kufunga mabao sita kwenye Ligi ya Championship msimu huu.

Kyaruzi akiwa sehemu ya kikosi cha Mtibwa Sugar msimu huu katika Ligi ya Championship ameiwezesha kuwa bingwa na kupanda daraja kurejea Ligi Kuu baada ya kushuka msimu uliopita. Mtibwa Sugar ilimaliza kileleni kwa pointi 71.

Timu hiyo ilishinda michezo 22 kati ya 30, sare tano na kupoteza tatu huku ikifunga mabao 58 na kuruhusu 18, ikiwa ni timu iliyoruhusu mabao machache na kushinda mechi nyingi zaidi (22).

Kyaruzi aliyewahi kutamba Ligi Kuu akiwa na timu za Kagera Sugar, Polisi Tanzania na Kagera Sugar, aliifungia Mtibwa Sugar mabao sita na kushika nafasi ya nne ndani ya kikosi hicho nyuma ya kinara, Raizin Hafidh (18), Fredrick Magata, Anuary Jabir na Omary Marungu wenye mabao manane kila mmoja.

Kyaruzi ambaye amemaliza mkataba wa mwaka mmoja aliosaini na Mtibwa Sugar, aliliambia Mwanaspoti kuwa umoja uliokuwapo ndani ya timu hiyo ndiyo ulikuwa msukumo mkubwa wa kufanya vizuri.

“Nashukuru kwa kutimiza lengo tulilopewa, haikuwa rahisi tumepambana kwa umoja na tumemaliza salama, kinachofuata Ligi Kuu sasa tunamuachia Mungu kwa sababu kwa sasa mimi ni mchezaji huru,” alisema Kyaruzi.

Alisema licha ya msimu kuisha mapema na kuwa huru hajabweteka kwani kwa sasa anaendelea kujifua ili kuwa fiti na kuwa tayari kupokea ofa zitakazojitokeza.

“Nipo naendelea na mazoezi, namuomba Mungu tu ofa yoyote ikija nisikilize japokuwa nimewapa nafasi Mtibwa Sugar kama watahitaji huduma yangu,” alisema beki huyo.