Noela, Juliana wachuana kwa asisti

Muktasari:
- Noela ambaye msimu uliopita aliichezea Vijana Queens, msimu huu ameonyesha kiwango kizuri akiwa na Jeshi Stars, huku Juliana Sambwe wa Tausi Royals anayecheza nafasi ya namba 1 (Pointi Guard) ni pili akiwa na asisti 31.
WAKATI ushindani kwa timu za wanawake ukizidi kushika kasi katika Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (WBDL), kwa upande wa asisti, Noela Uwendameno kutoka Jeshi Stars anaongoza kwa kutoa 34.
Noela ambaye msimu uliopita aliichezea Vijana Queens, msimu huu ameonyesha kiwango kizuri akiwa na Jeshi Stars, huku Juliana Sambwe wa Tausi Royals anayecheza nafasi ya namba 1 (Pointi Guard) ni pili akiwa na asisti 31.
Wachezaji wengine ni Jesca Lenga (DB Troncatt0-28), Tumaini Ndossi (Tausi Royals-22) na Elina Sinamenga (Twalipo Queens-22)
Kwa upande wa kunyakua mipira (Steal), Sambwe anaongoza kwa kufanya hivyo mara 14, akifuatiwa na Salma Sandali wa Vijana Queens (9).
Wachezaji wengine ni Elina Sinamengo wa Twalipo Queens (8), Mahewa Matema, Tausi Royals (8) na Noela Uwendameno, Vijana Queens (8).
Steal ni neno linalotumika baada ya mchezaji kunyakua mpira kutoka kwa mpinzani wake bila ya kumfanyia madhambi.
Katika ribaundi anayeongoza ni Taudencia Katumbi wa DB Lioness aliyedaka mara 74, akifuatiwa na Jacklini Mgaiwa wa City Queens (57).
Wengine ni Marshallet Shimbweche wa Reel Dream (53), Anamary Cyplian wa Jeshi Stars (48) na Nadjima Manji wa Ukonga Queens (45).