Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kwasi aanza kulipwa kwa mafungu

KLABU ya Tabora United imeanza kumlipa aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Asante Kwasi ikiwa ni siku chache tu tangu mchezaji huyo afungue mashtaka ya kuidai fedha zake za usajili hivyo kusababisha kufungiwa kusajili na FIFA.

Nyota huyo wa zamani aliyewika na timu za Simba, Mbao na Lipuli alipeleka malalamiko yake FIFA ya kutolipwa fedha zake za usajili tangu alipojiunga nayo msimu uliopita baada ya kuachana na klabu ya Hafia ya Guinea.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Thabit Kandoro alisema kabla ya kupewa barua ya kufungiwa kusajili kutokana na madai hayo, tayari walishaanza kumlipa nyota huyo fedha zake anazowadai.

“Siwezi kusema kiasi anachotudai kwa sababu ni makubalino binafsi ila tulishaanza kumlipa na hadi kufikia keshokutwa tutammalizia, lengo ni kuondokana na hiyo adhabu ambayo kwetu inatuletea taswira mbaya,” alisema.

Kwa upande wa Kwasi akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu kutoka Ghana alisema; “Nisingependa kuongelea mambo ambayo tayari yalishatolewa ufafanuzi na hukumu, kwangu sina shida na mtu yeyote, kwa sasa sina timu yoyote na matumaini yangu siku moja nirudi tena Tanzania.”