Kuziona Simba, Yanga buku kumi tu!

Tuesday September 21 2021
KIINGILIO PIC
By Charity James

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa mahasimu wa jadi, Simba na Yanga unaotarajia kuchezwa Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam Septemba 25, kitakuwa Sh10, 000.

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo alisema tiketi zimeshaanza kuuzwa na ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha mashabiki wa timu zote kununua mapema ili kukwepa usumbufu siku ya mchezo.

Alisema VIP A ni eneo maalumu ambalo limetengwa kwaajili ya wageni waalikwa maalum kutoka pande zote mbili huku akiweka wazi kuwa VIP B ni 30,000, (Buku 30 pekee) na ile VIP C ikiwa ni 20,000, mzunguko 10,000.

Mchezo huo itachezwa majira ya saa 11:00 jioni na wenyeji wa mchezo huo ni Simba ambao pia ni mabingwa watetezi wa ngao hiyo baada ya msimu uliopita kuifunga Azam FC.

“Maandalizi kwa upande wa Shirikisho kuelekea mchezo huo yemekamilika sasa tunawaachia Simba na Yanga wamalizie palipo baki zikiwa ni

dakika 90 za kuamua nami ataibuka mshindi,” alisema.

Advertisement
Advertisement