Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kola kuiongoza Azam FC dhidi ya Wasomali

MSHAMBULIAJI mpya wa Azam FC Rodgers Kola, ameanza kwenye kikosi cha wachezaji 11, akichukua nafasi ya Idris Mbombo atakayeanzia benchi.

Kikosi kamili kinachoanza dhidi ya Hosserd ni Mathias Kigonya, Nickolas Wadada, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Lusajo Mwaikenda, Sospeter Bajana, Ismail Aziz, Salum Abubakar 'Sure Boy', Rogders Kola, Paul Katema na Seleman Idd Nado.

Wachezaji wa akiba ni  Mohamed Salula, Abdul Haji Hamahama, Edward Manyanya, Abdallah Sebo, Frank Domayo, Mudathir Yahaya, Ayub Lyanga na Idris Mbombo.

Azam Fc inaikabili Hosserd kutoka Somalia katika mchezo wa marudiano unaopigwa katika Uwanja wa Azam Complex Chamanzi huku timu hiyo ikiwa na faida ya kuongoza kwa mabao 3-1, katika mchezo wa awali.