Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha wa Yanga afunguka kuhusu Dabi

Muktasari:

  • Hamdi alisema wachezaji wana kazi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara na ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) ili wapate matokeo mazuri, huku akisisitiza wako tayari kwa ajili ya kuendeleza rekodi ya ushindi kama walivyoanza.

WAKATI joto la pambano la Dabi ya Kariakoo likiendelea kupanda kwa mashabiki wa soka nchini, Kocha wa Yanga, Miloud Hamdi amevunja ukimya na kuweka bayana kwamba kwa sasa anaendelea kuwaandaa wachezaji kwa mechi tatu zilizosalia kufunga msimu kwa timu hiyo, lakini dabi haipo.

Hamdi alisema wachezaji wana kazi kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara na ya fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) ili wapate matokeo mazuri, huku akisisitiza wako tayari kwa ajili ya kuendeleza rekodi ya ushindi kama walivyoanza.

Kocha huyo aliwataja Pacome Zouzoua na Khalid Aucho kuwa wamerudi katika ushindani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wakiuguza majeraha waliyoyapata na kuwafanya wakosekane kwenye baadhi ya mechi zilizopita.

Kwa mujibu wa Hamdi, Yanga inaendelea kujifua kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons ugenini Juni 18 na kumalizia nyumbani na Dodoma Jiji Juni 22 kisha fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Singida BS huku mechi dhidi ya Simba ikiondolewa kwenye ratiba ya Yanga.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya katika mechi mbili za ligi ambazo zimebaki. Tunaamini zitakuwa ngumu kutokana na timu ambazo tunakutana nazo kuhitaji ushindi pia hasa wenyeji wetu kwenye mchezo wa kwanza ugenini haipo kwenye nafasi nzuri inahitaji pointi tatu ili kujiweka katika mazingira ya kucheza na sisi tunazihitaji ili tutetee taji,” alisema Hamdi.

“Kikubwa kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati, ninaamini kwamba tutafanya vizuri na kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu zijazo kikubwa kinachonipa matumaini ni kurejea kwa wachezaji wangu ambao hata hivyo tayari wamerudi kwenye ushindani.”

Hamdi alisema ukiondoa wachezaji walioitwa timu za taifa na beki Yao Kouassi aliye majeruhi, wengine wote wapo kwenye hali nzuri na tayari kupambania pointi sita.

“Morali ipo juu na wanaendelea vizuri na maandalizi Juni 18 tutakuwa ugenini kuikabili Tanzania Prisons hautakuwa mchezo rahisi, lakini nina imani kubwa na jeshi langu lote lipo timamu isipokuwa Yao na tunaombea walioitwa timu za taifa warejee salama,” alisema.

“Kurejea kwa Pacome na Aucho kumeongeza nguvu ukizingatia kuna mchezaji mmoja muhimu pia ameondoka kikosini Stephane Aziz Ki.” Hamdi alisema ukiondoa mechi mbili za ligi pia ile ya fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida Black Stars ambayo utachezwa kati ya Juni 26 hadi 28 wanaitaka.

“Sio mechi mbili tuna fainali moja pia ni muhimu kwetu tunahitaji mataji yote, hivyo kazi kubwa ni kwangu kuandaa mikakati sahihi na wachezaji kumaliza kwa kutumika vizuri dakika zote za mchezo na kuipa matokeo mazuri timu.”