Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha U17 sasa aipigia Uturuki hesabu kali huko

Muktasari:

  • Milambo aliongeza kuwa hataki kwenda kuwa mshirki badala yake kuwa mshindani, huku akiamini wachezaji wake watazidi kukomaa.


TIMU ya Taifa Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeweka kambi mkoani Arusha wakifanya maandalizi kwaajili ya mashindano ya UEFA Assist ambayo Serengeti anaenda kama mwalikwa.

Timu hiyo ilianza kuweka kambi jijini Dar es Salaam sasa imehamishiwa jijini Arusha ambapo Kocha mkuu wa Serengeti Boys, Oscar Milambo aliliambia Mwanaspoti sababu za kukimbilia huko ni kuzoea hali ya hewa ya baridi kabla ya kutimkia Uturuki ambako pia hali ya hewainaendana na huko.

“Hapa kuna baridi na huko (Uturuki) kuna baridi, tunaporajaria kwenda kama wiki mbili mbele vijana wanatakiwa waanze kuzoea hali ya hewa hii kabla hatujaenda kukutana nayo kule,”alisema.

Milambo aliongeza kuwa hataki kwenda kuwa mshirki badala yake kuwa mshindani, huku akiamini wachezaji wake watazidi kukomaa.

“Wachezaji wana morali nzuri na lengo ni kuhakikisha tunaenda kupambana, maandalizi ni mazuri tunaendelea kupambana kuona tunafanikiwa,” alisema.