Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Serengeti Boys aukwaa Ukurugenzi wa Ufundi TFF

Muktasari:

Oscar Mirambo lilianza kuvuma kwenye soka wakati alipokuwa Kocha Mkuu wa Shule ya Vipaji ya Makongo ambayo imezalisha idadi kubwa ya wanasoka nchini.

Dar es Salaam. Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana Tanzania chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti Boys', Oscar Mirambo, ametangazwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu aliyekuwa akiishikilia, Ammy Ninje kuondoka baada ya kuvunjika kwa mkataba baina yake na TFF mara baada ya kumalizika kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alisema kuwa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo imeamua kumpitisha Mirambo kwa sababu ana sifa stahiki za kuhudumu kwenye nafasi hiyo.

"Kwanza ni kijana, lakini kubwa zaidi ana elimu kubwa kuanzia kwenye soka hadi ile ya kawaida ambapo yeye ni msomi mwenye shahada ya Uzamili ya takwimu huku shahada yake ya kwanza ikiwa ni ya elimu ambayo aliipata kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

“Pia ni kocha mwenye leseni B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na ameinoa timu ya taifa ya vijana 'Serengeti Boys' ambayo ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na ule wa Kusini mwa Afrika ambao tulialikwa," alisema Kidao.

Kidao alisema shirikisho hilo lina imani kubwa na Mirambo kufanya vyema katika nafasi hiyo.