VIDEO: Makocha kuwaona Serengeti Boys

Muktasari:

Bares amesema, suala la Serengeti Boys ni la Watanzania wote kwani mafanikio yatakayopatikana ni ya wote.

MAKOCHA wa Ligi Kuu na wengine wameshauriwa kupita na kutoa michango yao mbalimbali kwa kikosi cha timu ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' lakini TFF nayo imewaambia iwaunge mkono walimu wao.
Ushauri huo umetolewa na Kocha wa Mlandege ya Zanzibar na Klabu za Tanzania Prisons pamoja na Ndanda FC, Abdallah Mohammed 'Bares'.
Bares amesema, suala la Serengeti Boys ni la Watanzania wote kwani mafanikio yatakayopatikana ni ya wote.
"Kitu cha kwanza ambacho nashauri kama upo uhuru, makocha wapite kuwaona vijana na kutoa michango yao mbalimbali ambayo itasaidia timu kufanya vizuri,"alisema Bares.
"Pia, TFF iruhusu maana naweza kusema hivyo kumbe kuna katazo. Serengeti Boys ni yetu sote."
Amesema, yeye ameshindwa kufika kwa sababu yuko mbali Kisiwani  Zanzibar ambako pia ana majukumu na klabu yake ya Mlandege.
"Kama ningekuwa karibu ningefika bila kujali jambo lolote lakini ni kwa sababu ya majukumu tu.