Serengeti Boys, Australia hapatoshi leo

Muktasari:
- Timu nane zitashiriki fainali hizo ambazo ni Uganda, Angola, Nigeria, Cameroon, Senegal, Morocco, Guinea na wenyeji Tanzania.
Dar es Salaam.Baada ya juzi kuanza vibaya michuano ya Uefa Assist, timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' inatupa karata nyingine itakapovaana na Australia leo saa 9:30 Alasiri.

Timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys wakiwa kwenye mazoezi mepesi ya kutembe barabarani nchini Uturuki, timu hiyo inashiriki mashindano ya Kimataifa ya UEFA ASSIST kujiandaa na Fainali za Afrika za Vijana U17.
Serengeti Boys ilipoteza mechi ya kwanza kwa kufungwa bao 1-0 na Guinea mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Emirhan Sports Complex mjini Antalya.
Bao la Guinea katika mchezo uliochezwa kukiwa na baridi kali lilifungwa na Abubakar Konte dakika ya 26.

Timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys wakiwa kwenye mazoezi mepesi yUwanja wa Tenis nchini Uturuki,timu hiyo inashiriki mashindano ya Kimataifa ya UEFA ASSIST kujiandaa na Fainali za Afrika za Vijana U17 mwezi Aprili.
Serengeti Boys leo ina nafasi nyingine ya kusahihisha makosa na kupata ushindi dhidi ya Australia kama itakuwa na nidhamu ya mchezo.
Tanzania imepangwa Kundi A katika michuano hiyo maalumu na timu za Guinea, Australia na Uturuki. Kundi B Uganda, Morocco, Belarus na Cameroon. Kundi C Angola, Nigeria, Senegal na Montenegro.

Timu ya Taifa ya Vijana U17 Serengeti Boys wakiwa kwenye mazoezi mepesi ya Uwanja wa Tennis nchini Uturuki.
Serengeti Boys inatumia michuano hiyo kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 zitazofanyika Dar es Salaam kuanzia April 14 hadi 28.
Timu nane zitashiriki fainali hizo ambazo ni Uganda, Angola, Nigeria, Cameroon, Senegal, Morocco, Guinea na wenyeji Tanzania.