Kocha Mbeya City apania kuwaadhibu wajeda

Friday November 20 2020
mbeya city pic

Kocha msaidizi wa Mbeya City, Mathias Wandiba amesema anamaini vijana wake wataendeleza ari ya kupambana wanapoikabili Ruvu Shooting leo na kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu muhimu.

Mbeya City itakuwa ugenini leo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kucheza na Ruvu Shopoting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa timu hiyo katika mechi tatu zilizopita ndicho kinampa jeuri kocha Wandiba ambaye anaamini hata katika mchezo wa leo watafanya vizuri.

Tangu Wandiba akabidhiwe timu hiyo ameiongoza Mbeya City katika michezo mitatu, akishinda mmoj na kutoka sare miwili hivyo anaamini wachezaji wake wameendelea kuimarisha viwango vyao hivyo hata mchezo wa leo wana uwezo wa kuibuka na ushindi.

"Tangu nikabidhiwe kijiti cha kuiongoza timu hii jambo la kwanza nililofanya ni kuwajenga kwanza wachezaji wangu kisaikolojia ili wajue kuwa wana uwezo mkubwa wa kupambana na timu ikapata matokeo hivyo muhimu ni kujitoa tu uwanjani.

"Nashukuru wamenielewa na kadri muda unavyokwenda wameendelea kuimarika na kucheza vizuri", amesema Wandiba.

Advertisement

Akizungumzia mchezo wa leo Novemba 20 dhidi ya Ruvu Shooting, Wandiba amesema" Najua nakutana na timu ngumu yenye kocha mzuri(Charles Mkwasa) mwenye ufundi mwingi hivyo lazima nijipange sana lakini nina uhakika kutokana na ubora tulionao tutapata pointi tatu".

______________________________________________________

By Oliver Albert


Advertisement