Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Kerr apata kombinesheni mpya

Muktasari:

Awali Kerr alikuwa na Hassan Isihaka na Juuko Murshid katika beki ya kati wakati ambapo beki mpya Mohamed Faki akiwa bado anauguza majeraha ya goti aliyopata mwishoni mwa mwezi Julai.

KOCHA wa Simba, Dylan Kerr, amesema amepata kombinesheni mpya ya mabeki wa kati ambayo inaundwa na Mzimbabwe, Justice Majabvi na chipukizi Said Issa.

Kerr alisema Issa ameonyesha kiwango cha kuvutia katika mechi mbili za kirafiki walizocheza visiwani Zanzibar, hivyo kumpatia wigo mpana sasa wa uchaguzi katika nafasi hiyo ya beki huku akimtaja Majabvi kama mchezaji pekee katika kikosi chake anayeweza kucheza katika eneo analohitaji.

Awali Kerr alikuwa na Hassan Isihaka na Juuko Murshid katika beki ya kati wakati ambapo beki mpya Mohamed Faki akiwa bado anauguza majeraha ya goti aliyopata mwishoni mwa mwezi Julai.

“Issa ndiye mchezaji aliyefanya vizuri zaidi katika mechi zangu mbili za kirafiki za mwishoni, amekuwa akifanya makosa machache na baada ya hapo anakwenda kuyarekebisha haraka, anakuja kwa kasi sana huyu kijana,” alisema.

“Majabvi ni mchezaji mwenye uzoefu na uwezo mkubwa, anaweza kucheza sehemu yoyote ninayohitaji acheze uwanjani.”