KMC yatamba kufanya makubwa

KMC imetamba kufanya mazuri mbeleni baada ya kuanza vibaya Ligi Kuu na sasa inatamba kufanya makubwa mechi zijazo.

Timu hiyo ilianza kwa kutoa sare ya bao 1-1 na Namungo ugenini kisha kuchapwa mabao 5-0 na Yanga na kumaliza mechi mbili na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania na Geita Gold ugenini.

Winga wa timu hiyo, Tepsie Evans alisema wao kama wachezaji walitolewa mchezoni baada ya kufungwa na Yanga lakini benchi lao la ufundi limewasaidia kuwarudisha katika hali ya morali na sasa wanaendelea vizuri.

Alisema sasa wamejipanga vizuri na haikuwa rahisi kuwafunga Geita nyumbani kwake lakini wanaamini morali walionayo itawasaidia kuendelea kupata matokeo mazuri.

"Tulianza vibaya mechi mbili za kwanza, maneno ya watu kwamba tuna timu mbovu yalitutoa mchezoni lakini sasa tumerudi vyema na tunaamini tunajipanga vyema kwaajili ya mechi zijazo." Alisema Tepsie